WAHARIRI TANZANIA NI SIKIO LA KUFA ,WACHARAZA WAPEWA DOZI YA BAKORA NA WANAHABARI IRINGA
 Mchezaji wa timu ya  wanahabari Iringa Lukelo Mkami kushoto akiteta  jambo na mlinda mlango wa akiba wa timu ya  wahariri 
 Kikosi cha  wanahabari Iringa  waliovalia  uzi wa yanga  
 Mgeni  rasmi  mwenyekiti wa  jukwaa la wahariri  Bw  Kibanda akizungumza na  wachezaji kabla ya mchezo  kuanza 
 Timu ya   jukwaa la wahariri  kulia 
yenye  uzi wa simba  ikiwa na timu ya  wanahabari  mkoa  wa Iringa kabla
 ya  mchezo kuanza  uwanja wa samora  jana 
 Kikosi cha  wanahabari  Iringa  kilichoanza  kazi  
 Mgeni  rasmi katika mchezo huo mwenyekiti  wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,akisalimiana
 na  wachezaji  wa  timu ya  wanahabari mkoa  wa Iringa katikati ni 
katibu wa IPC Francis Godwin akisaidia  kutambulisha wachezaji hakuna 
mamruki  hapa 
 Kikosi  imara  kweli kweli japo si wote  wapenzi wa Yanga ila voda Com imetuweka pamoja 
 Kiongozi  wa timu ya  jukwaa Kulwa 
Karedia  kulia akimtambulisha mgeni rasmi mwenyekiti wa jukwaa Bw 
kibanda  wachezaji wa  timu yake iliyochezea bakora 
 MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,akiwa na mchezaji wa wanahabari Iringa Lukelo Mkami 
 MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,
 kulia akiwa na  wachezaji wa  timu  zote  mbili kabla ya mchezo na 
kushoto ni mwalimu wa  timu ya jukwaa la  wahariri Bw Masoud 
 Hili  ndilo goli la pekee kwa  wanahabari Iringa 
 Wanahabari  wakifuatilia  mchezo huo 
 Mlinda  mlango wa Jukwaa akiwa hoi  baada ya  kuchezewa vibaya  
 Wachezaji  wa akiba Swiga  Mwaisumbe 
kocha wa  timu ya  wanahabari Iringa  na Francis Godwin katikati pamoja 
na mbunge Peter Msigwa  wakijiandaa kwa  kupasha kabla  ya  kuingia  
uwanjani kipindi  cha pili 
 Hapa  wachezaji  wa akiba  Swiga Mwaisumbe  kulia ,mbunge Peter Msigwa na Francis Godwin  wakipasha 
 Mzee  wa matukio  daima jezi nnamba  7 
akiwajibika  uwanjani baada ya  kuingia  kipindi  cha pili  huku mwamuzi
 wa mchezo huo Frederick Mwakarebela kushoto akikimbia kuufuata mpira 
 Washambuliaji hatari mzee  wa matukio  
daima namba 7  ,mbunge Msigwa namba 2 kushoto na Raymond Francis mwenye 
rasta  wakiwajibika vema 
 Mbunge Msigwa akijiandaa kupiga mpira japo hakuweza kuingiza nyavuni 
 katibu  wa IPC Francis Godwin kulia 
akiwashukuru  wadhamini wakuu Voda Com , Frederick Mwakalebela  na  Asas
 kwa  kudhamini mchezo huo katikati ni mwenyekiti  wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibandaaliyekuwa mgeni  rasmi na makamu Rais  wa UTPC Jane Mihanji 
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Bw Kibanda baada ya timu ya wanahabari Iringa kushinda mchezo huo .
TIMU ya jukwaa la wahariri wa habari Tanzania (TEF) imekuwa ni sawa na sikio la kufa ambalo kamwe halisikii dawa baada ya kukubali kupokea tiba ya bakora moja kutoka kwa wanahabari mkoa wa Iringa .
katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Samora Iringa jana ,mchezo uliojaa vionjo vya kila aina kutoka kwa timu zote mbili pamoja na mwamuzi wa mchezo huo aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela timu hizo ziliweza kuvunja mbavu za mashabiki uwanjani hapo.
Wakati wachezaji wa timu ya wanahabari Iringa baada yao wakionyesha kujikata chenga wenyewe kwa wenyewe ,timu ya jukwaa ambayo ilikuwa na wachezaji waliokula chumvi nyingi huku baada yao wakishindwa kukimbia kutokana na vitambi walivyokuwa navyo bado kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya timu hizo kuona nyavu ya mwingine.
kipindi cha pili timu zote vilifanya mabadiliko makubwa zaidi kwa kuwatoa wachezaji karibu ya nusu ya wali waliocheza kipindi cha kwanza na kuweka wapya hali iliyoonekana ni ngumu zaidi kwa jukwaa la wahariri na nyepesi kuliko kwa wanahabari Iringa ambao waliweza kutumia mabadiliko hayo kuwacharaza bakora wahariri hao .
Wanahabari Iringa wakicheza kwa nguvu zote kipindi cha pili walipata bao la kuongoza na kufungia dimba dakika ya 3 kipindi cha pili goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Awali katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) mkoa wa Iringa Francis Godwin alisema kuwa mbali ya timu yake kushinda ila ushindi huo ni mwembamba sana na kuwa walipendezewa kuichapa timu hiyo ya jukwaa la wahariri kwa jumla ya magoli 5-0.
Hata hivyo aliwashukuru wadhamini wa mchezo huo ikiwemo kampuni ya simu ya Voda Com kwa kudhamini mchezo huo kwa asilimia 100 ,mdau wa michezo mkoa wa Iringa Frederick Mwakalebela aliyetoa zawadi ya ng'ombe kwa mabingwa wa mchezo huo timu ya wanahabari mkoa wa Iringa pamoja na jukwaa la wahariri kwa kuamua kuja kucheza na wanahabari mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mchezo huo mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alisema kuwa mbali ya timu yake kufungwa ila bado wanahabari Iringa wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa wahariri hao.
Kwani alisema kuwa jukwaa la wahariri kila mwaka limekuwa na mkutano mkuu wa mwaka na kufanyika katika mikoa mbali mbali na mwaka huu wamechagua Iringa kuja kufanya mkutano wao na kucheza mchezo huo wa kirafiki na wanahabari wa mkoa wa Iringa.

Post a Comment