WAPENZI WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, WATOSHEKE?
Kwa
wiki nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali
ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki
tendo la ndoa na kulidhika.
Wengi
kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea
waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki
kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke?
Jibu
la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho
ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo
zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani
kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza
wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali kwenye
akili ya mtu.
Kwa
msingi huo mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima
kwanza aitosheleze akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo
atalifikia kwa kutathimini uwezo wake wa kufanya mapenzi na wa mpenzi
wake. Wengi kati ya watu wanaodai hawatosheki kimapenzi ni wale
wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo,
nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Nikijibu
swali la ni mara ngapi wapenzi wakutane kimwili ili watosheke nitasema
hivi: KUTOSHEKA HAKUNA IDADI, bali ni kwa kila mmoja kulidhika na mwenza
wake kutoka ndani ya akili yake. Kama hapa sikueleweka vizuri katika
jibu hilo, maana yangu hasa ni kwamba kutosheka ni namna mtu mwenyewe
anavyoyaendesha mawazo yake.
Ukiyaendesha
mawazo yako kufanya mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa
kila saa, kwa sababu fikra zako unazijenga zaidi ya unachopata.
Uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao akili zao zimejaa mawazo ya ngono,
hawawezi kulala bila kufanya mapenzi, lakini watu hao hao, ukiwapa
matatizo yatakayochukua sehemu kubwa ya mawazo yao kwa mfano, kuwafunga
jela, kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa wanaweza kukata wiki
bila kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii
ina maana kwamba unavyowaza ndivyo unavyotenda. Kitaalamu kinachofanya
mapenzi ni mawazo, ndiyo maana wapo wanaojichua wenyewe kwa kutumia
mawazo yao na kupata raha. Kila mmoja akijenga heshima juu ya fikra zake
na kujali hisia zaidi tutakuwa na watu wengi wanaofurahia tendo la ndoa
bila kujali wanalipata mara ngapi kwa wiki.
Uchunguzi
wangu umebaini kuwa watu wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na wanandoa,
wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini
si kwa kuheshimu fikra na hisia zao, jambo ambalo husababisha ladha ya
mapenzi kuwa ya asilimia ndogo, ukilinganisha na mahitaji halisi ya
mawazo yao.
Upo
ushahidi wa kutosha kwa wanandoa wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa
na waume/wake zao katika tendo la ndoa tofauti na wanapopata wasaa wa
kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu
wa aina hii wasiseme kuwa hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu
wanakutana na wapenzi wao mara chache zaidi, bali wanakutana katika
mhemko wa chini usioweza kulifanya tendo hilo kuwa na raha ya kutosha.
Labda
msomaji wangu utaniuliza, tatizo la kupata msisimko mdogo kwa mtu
unayemzoea linachangiwa na nini? Jibu litakuwa ni MAWAZO ya mtu
mwenyewe.
Ukichunguza utagundua kuwa, wapenzi wengi hasa wazoefu huwa hawapeani nafasi katika mawazo, kamawanavyotoa
nafasi kwa wapenzi wa pembeni, hili ndilo tatizo linalopunguza msisimko
wa kimapenzi na kuondoa hali ya kutosheka na penzi. Kama mtu anataka
mpenzi wake amtosheleze, basi hana budi kumkuzia mwenza wake hisia kiasi
cha kumtamani. Niulize swali, hivi ni mara ngapi wewe unayesema
hutosheki na penzi ulishakaa peke yako ukamvutia taswira mpenzi wao
kabla hajarudi nyumbani kiasi cha kupata msisimko wa kutana naye
kimwili?
Wengi
wetu hatufanyi hivyo, hatuna vitu vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu,
jambo ambalo hutufanya tukikutana nao kimwili kwa kutimiza desturi tu na
kubaki na kiu zetu za penzi. Lakini uweli unabaki kuwa wapenzi
wakikutana kipindi cha msisimko mkubwa na kupeana mahaba kwa usahihi
hata ikiwa ni mara moja kwa wiki watatosheka.
Jambo
kubwa la kuzingatia hapa ni kwamba wakati mwingine msisimko huo huwa
hauwatokei wapenzi kwa wakati mmoja, hivyo ni jukumu lao kushirikiana
pindi mmoja anapokuwa katika hali hiyo.
WAPENZI WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, WATOSHEKE?
Reviewed by crispaseve
on
11:00
Rating:
Post a Comment