Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi halisia
cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu nchini
Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa.
Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.
Taarifa ambazo BC imezipata zinapasha kwamba Mzee Sepetu ambaye kwa
muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi ya
kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki
jijini Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa
marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo
miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu
Julius Kambarag Nyerere. Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi
tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa
Zanzibar, Dr Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

Post a Comment