PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.
Meneja
wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akibonyeza kitufe cha kuchezesha
droo ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mapema leo katika ofisi za
Kiwanda cha Bia chaa Serengeti jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa
na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari
Maggid(kushoto) na Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora(kulia).
Meneja
wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza na wana habari wakati wa
droo ya saba ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti
inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha
droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
na kulia kwake ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Bakari Maggid.
PROMOSHENI
YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.
Washindi
Zaidi kupatikana, zawadi za ving’amuzi na simu za kisasa zazidi kutolewa!
26 Machi, 2014: katika
hafla fupi mapema leo kampuni ya bia ya Serengeti imeendelea kuchezesha droo
zake za winda safari ya Brazil na Serengeti na leo washindi wawili wa simu za
kisasa aina ya Samsung galaxy tablet wamepatikana.
Kwa mtu kujishindia zawadi
zetu unahitaji kununua chupa ya bia ya Serengeti na kuangalia chini ya kizibo
ambapo utakuta bia ya bure au tarakimu 6 ambazo utazituma kwa ujumbe mfupi
kwenda namba 15317 ambapo utapata ujumbe ukikujulisha kama umejishindia fedha
taslimu kati ya shilingi 5000 na shilingi 10000 na pia namba yako itaingizwa
katika droo ambapo utaweza kujishiandia king’amuzi, simu ya mkononi au tiketi
ya kwenda Brazil.
Mji wa moshi
katika maeneo ya majengo umepata bahati ya kutoa washindi wawili wa simu aina
ya Samsung tablet. Juma lililopita katika droo ya 6 ya winda safari ya Brazil
washindi wawili waliopatikana wote wanatokea katika maeneo ya Majengo Moshi.
Droo hiyo ilishuhudiwa na waandishi wa habari, ofisa kutoka bodi ya michezo ya
kubahatisha, PWC pamoja na Push mobile media. Droo kubwa itatoa tiketi ya
kwenda Brazil ambaponmshindi atalipiwa gharama zote kwa siku atakazokaa huko.
Meneja wa bia ya
Serengeti Bw Rodney Rugambo aliongea na mshindi wa kwanza Bw Matei Kleti Mofulu
kutoka Nyakato, Mwanza. Akiwa na furaha muda wote wa maongezi alisema hajaamini
kama ameshinda na amekuwa akiamini michezo hii siyo ya ukweli ila Serengeti
wamemfumbua macho kuwa ni za kweli.
Mshindi wa pili pia alipokea habari hizi
kwa furaha na kusema kuwa ni muda kuwa wa kisasa kwa kutumia simu ya kisasa.
Pia mshindi wa pili wa simu ya kisasa Bw Godwin Paul ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ
aliishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa zawadi hiyo na kuwashauri watumiaji
wa Serengeti kushiriki katika promosheni hii.
Tafrija fupi za
kugawa zawadi kwa washindi zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania
ambapo katika juma lililopita mshindi wa simu ya kisasa wa Dar es Salaam
alikabidhia zawadi yake katika maenao ya kimara. Mshindi huyo Bw Erick Mazigo
alishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa waaminifu kwa wateja wao na
kuwapa zawadi zao. Promosheni ya winda safari ya
Brazil ambayo imekuwa gumzo nchi nzima imeshapata washindi Zaidi ya 100000 wa
bia za bure, Zaidi ya washindi 13000 waliojipatia fedha taslimu shilingi 5000
na 10000.
Kunywa
kistaarabu; washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa Zaidi ya miaka 18; vigezo na
masharti kuzingatiwa.
PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.
Reviewed by crispaseve
on
00:29
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
00:29
Rating:



Post a Comment