Makomandoo
wa Vicent Calderon, Timu ya Atletico Madrid imejikuta ikilazimishwa
sare nyumbani kwao na vijana wa darajani ‘Chelsea’ na kufanya matokea
kuwa bila bila ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya
michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Mchezo
huo uliokuwa wa vuta ni kuvute kwa kila pande ingawa kwa upande wa
Chelsea hali ilikuwa tete kufuatia kuumia kwa kipa Peter Cech na kapteni
wa kikosi hicho ‘John Terry’ aliyeshindwa kuendelea na mchezo huo na
kumlazimu kutolewa..
Hapo
kesho kunako majaliwa, Real Madrid itawakaribisha kwenye dimba lao la
Stantiago Bernabeu Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa pili
wa hatua ya nusu fainali.
ATLETICO MADRID YATOKA SARE TASA NA CHELSEA
Reviewed by crispaseve
on
00:22
Rating: 5
Post a Comment