CHINA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKATABA WENYE THAMANI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na. Benedict Liwenga-MAELEZO.
16/05/2014
OFISI
ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo imetialiana saini
na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya
Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament)
wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Utaiji
saini huo umefanyika leo katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ukihusisha viongozi wa pande zote mbili akiwemo
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha
na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association
for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani
utasaidia ofisi ya Bunge kuweza kupata vifaa mbalimbali vya ofisi
vikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu, vipaza sauti, kamera pamoja na
vifaa vya kurekodia.
“Ndugu
zetu kutoka China pamoja na hiki Chama chao wamesaini pamoja nasi
mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ambao wametutaka
sisi tuamue wenyewe ni vifaa gani tunahitaji kwaajili ya ofisi yetu ya
Bunge mjini Dodoma ili wao waweze kutununulia na kutukabidhi”. Alisema
Kashililah.
China
na Tanzania zimekuwa zikitiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo
ambayo kwa namna moja mikataba hiyo imekuwa ikizinufaisha pande zote
mbili kiuchumi na mpaka hivi sasa uhusiano huu umedumu kwa muda miaka
hamsin
CHINA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKATABA WENYE THAMANI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI
Reviewed by crispaseve
on
02:34
Rating:

Post a Comment