HALI YA SOKO LA KARUME YASIKITISHA MARA BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO ULIOANZA JANA USIKU
Baadhi
ya Wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Dar wakiwa katika soko la
karume kujionea hali ilivyokuwa mara baada ya kuteketea kwa moto
Moto ukiendelea Kuunguza mabati na vitu mbalimbali katika Soko hilo la Karume, Jijini Dar Es Salaam
Askari
wa Kikosi cha Zima Moto akiendelea na Zoezi la kuzima Moto katika Soko
la Karume lililoteketea kwa Moto ambao chanzo chake hakijulikani bado
Mmoja wa mfanyabiashara katika soko hilo hakikusanya mabati yake mara baada ya kuteketea kwa moto katika Soko la Karume
Wafanyabiashara
wakikukasanya mabaki ya mabati mara baada ya mabanda yao kuteketea kwa
moto uliowaka tokea usiku wa kuamkia leo katika Soko hilo la Karume.
Mfanyabiashara akiamisha baadhi ya mali alizoweza kuziokoa mara baada ya moto mkubwa kuteketeza soko la Karume.
Masanduku ya chuma yakiwa yameungua kabisa na moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya Soko la Karume.
Baadhi
ya wafanyabiashara waliokuwa na mabanda yao katika soko la Karume
wakiwa na nyuso za majonzo mara baada ya mabanda yao kuteketezwa kwa
moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya mali za wafanyabiashara.
Wakazi
wa Jiji la Dar Wakishuhudia jinsi kikosi cha Zimamoto kikiendelea na
zoezi la Uzimaji wa moto huo ambao umeendelea kuteketeza mali za
wafanyabiashara wa soko hilo.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza
Blog
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI»
HALI YA SOKO LA KARUME YASIKITISHA MARA BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO ULIOANZA JANA USIKU
Reviewed by crispaseve
on
14:05
Rating:
Post a Comment