Waziri Mkuu Pinda afungua Mkutano wa mawaziri wa mazingira na mambo ya nje
Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda (wa pili kulia
waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje
kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi
za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda( wa pili kulia
waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje
kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi
za Afrika wenye lengo la kujadili
changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi hizo leo jijini Dar es Salaam.(
Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia
Uchumi Vijijini na Kilimo Roda Tumusiime akizungumza na wajumbe ambao ni Mawaziri wa
Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi
kwa nchi za Afrika.
Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa
mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu
wa Nchi za Afrika akisoma risala ya ufunguzi wa
mkutano huo jijini Dar es Salaam wenye lengo la kupata muongozo wa
kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi za Afrika ili kuwasilisha
maazimio hayo katika mkutano unaotarajiwa kufanyika Septemba 23,2014 nchini
Marekani.
Waziri Mkuu Pinda afungua Mkutano wa mawaziri wa mazingira na mambo ya nje
Reviewed by crispaseve
on
13:14
Rating:
Post a Comment