Header AD

KWENU HAFAI, HUKU KIFAA, KAGAWA APIGA BAO, ATOA PASI YA BAO



Kungo Shinji Kagawa ameanza kuonyesha kuwa bado yuko safi licha ya kuonkana hana kiwango cha juu akiwa Man United.

Kagawa amefunga bao moja na kutoa pasi iliyozaa bao wakati Borussia Dortmund ilipoilaza Freiburg kwa mabao 3-1 katika Bundesliga.


Katika mechi hiyo, Dortmund wakiwa nyumbani walionyesha kiwango kizuri dhidi ya timu hiyo kutoka Kusini mwa Ujerumani.
Adrian Ramos alianza kufunga bao la kwanza katika dakika ya 34, Kagawa akafunga la pili katika dakika ya 41.

Lakini Kagawa tena akatoa pasi safi kwa Aubameyang aliyefunga la tatu katika dakika ya 78.

Wageni Freiburg walipata bao lao la kufutia machozi katika dakika ya 90 kupitia Oliver Sorg.
KWENU HAFAI, HUKU KIFAA, KAGAWA APIGA BAO, ATOA PASI YA BAO KWENU HAFAI, HUKU KIFAA, KAGAWA APIGA BAO, ATOA PASI YA BAO Reviewed by crispaseve on 00:37 Rating: 5

No comments

Post AD