MWANAMUZIKI RAPPA MAHIRI KUTOKA NCHINI MAREKANI T.I KUSAMBAZA UPENDO NDANI YA TAMASHA LA FIESTA OKTOBA 18,2014 JIJINI DAR

T.I atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini Dar.
Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika soko la muziki.
T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.
Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us" (FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).
MWANAMUZIKI RAPPA MAHIRI KUTOKA NCHINI MAREKANI T.I KUSAMBAZA UPENDO NDANI YA TAMASHA LA FIESTA OKTOBA 18,2014 JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
02:56
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
02:56
Rating:

Post a Comment