Wamiliki, Waombaji leseni za madini watakiwa kufuata Taratibu
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya leseni
za uchimbaji madini kwa wamiliki waliokidhi vigezo vya kuapatiwa leseni.
Anayeangalia ni Mwanasheria Wizara ya Nishati na MadinI Phines Sijaona.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza mmoja wa
waombaji wa Leseni za uchimbaji madini, Mark Stanely mmiliki wa kampuni
ya Bafex Tanzania Limited (Kanda ya Kusini Magharibi) wakati wa kikao
cha kusaini leseni za uchimbaji madini zilizokidhi vigezo
Kamishna
Msaidizi anayeshuhgulia Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
John Nayopa, akifafanua jambo wa wamiliki wa kampuni ya Gemini
Exploration & Mining Service Limited mara baada ya Waziri wa Nishati
na Madini, Sospeter Muhongo kumaliza kusaini leseni hizo.
Na
Asteria Muhozya, Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wamiliki na waombaji wa
leseni za kuchimba madini kuhakikisha
wanayaendeleza maeneo yao kwa kufanya kazi katika muda walioomba kulingana na leseni
hizo la sivyo watafutiwa leseni zao kwa
mujibu wa sheria ya madini.
Waziri
Muhongo ameyasema hayo wakati akisaini leseni za Kampuni mbalimbali zilizokidhi
vigezo vya kupatiwa leseni za uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali nchini
na kuongeza kuwa, kuanzia sasa Wizara haitaruhusu wamiliki wa leseni za madini kuuza
maeneo yao kwa wamiliki wengine na kubadilisha majina ya kampuni kutoka kwa
mmiliki mmoja kwenda mwingine badala yake itaruhusu endapo pande mbili zitaingia
ubia.
“Hatutakubali
wamiliki wa leseni kuuza maeneo yao na kubadili jina kutoka kwa mmliki mmoja
kwenda mwingine badala ya kuyaendeleza, lakini kama wanaingia ubia hilo
linakubalika” alisisitiza Muhongo.
Kauli
ya Waziri imekuja baada ya kubaini kuwa, baadhi ya wamiliki wa leseni za
uchimbaji madini kutokuyaendeleza maeneo yao kwa muda mrefu pindi wanapopewa
leseni na badala yake kuyauza na kubadili majina ya kampuni jambo ambalo
linachochea migogoro katika maeneo husika.
“Wananchi
wanategemea mara baada ya kampuni kupewa leseni waombaji waendeleze maeneo yao
lakini badala yake maeneo yanakaa bila kuendelezwa jambo ambalo linaibua
migogoro”, aliongeza Muhongo.
Aidha,
ameongeza kuwa, hatua hiyo inalenga kuwafanya waombaji na wamiliki kuwajibika na
kufanya kazi kisasa badala ya kufanya kwa mazoea. “Hatutaki waombaji wafanye
kazi kizamani, hatutaki kupotezeana muda katika hili”, alisisitiza Waziri.
Kampuni
zilizopata leseni za uchimbaji, ni pamoja na Bafex Tanzania Limited (Kanda ya
Kusini Magharibi) Autrad Mining Company Limited, Nyang’wale Diamonds Limited
(Kanda ya Kati Magharibi) na Paulo Sungura na Joyce Abinel Sekwao (Kanda ya
Magharibi).
Wamiliki, Waombaji leseni za madini watakiwa kufuata Taratibu
Reviewed by crispaseve
on
02:48
Rating:

Post a Comment