Header AD

JHIKOMAN, ZAWOSE, MAEMBE KUPAMBA ‘KARIBU FESTIVAL’

Px 1
Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
..Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole

Na Andrew Chale
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.

Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
px2
Mwanamuziki wa Msafiri Zawose anayepiga nyimbo za Cigogo, akionjesha vionjo vya moja ya nyimnbo zake kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho kwa wanahabari.

Makundi na majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band, Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa.

Wengine ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.
JHIKOMAN, ZAWOSE, MAEMBE KUPAMBA ‘KARIBU FESTIVAL’ JHIKOMAN, ZAWOSE, MAEMBE KUPAMBA ‘KARIBU FESTIVAL’ Reviewed by crispaseve on 02:16 Rating: 5

No comments

Post AD