LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGO
La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.
La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.
MWANADADA,
aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene
Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris
wameondoa gundu kwa ushindi wao.
Akizungumza
na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana na
washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,
“Binafsi
nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni
furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond
kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka
Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa
wasanii wa Kitanzania’, alisema.
Aidha
La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku
atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani
nzuri kimataifa.
Kujua zaidi Mahojiano aliyofanya La Veda baada ya kuwasili, usikose kutembelea www.globaltvtz.com
(PICHA / HABARI: Na Gabriel Ng’osha/GPL)
LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGO
Reviewed by crispaseve
on
01:54
Rating:

Post a Comment