NGOMA AFRICA BAND NA MZIMU WAO WA MZIKI WA DANSI ! WENYE MVUTO MKUBWA BARANI ULAYA

Bendi
maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,ni bendi ya
kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za
washabiki uko ughaibuni.
Bendi
hiyo ambayo imetajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia
muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake
katika kona zote duniani,pia imetajwa na vianzo vya habari vya
kimataifa kuwa mdundo wa mziki wake umekuwa ni urimbo unao wanasa na
kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani.
Bendi
ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani
ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja
almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU,Mtawala wa
himaya ya Anunnaki Empire "ambaye pia ndiye mtunzi,mwimbaji na kiongozi
wa bendi hiyo,bendi yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao
wakiwemo mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi”
wa solo gitaa ambae pia yupo katika safu ya uimbaji,Wengine ni Matondo
Benda,Aj Mbongo na Saidi Jazbo Vuai wapiga bass gitaa ,Jonathan Sousa
aka “Jo Jo” (Drum),wapo akina dada FrolaWilliam,Jessica Oyah ,bendi hiyo
maarufu ina wanamziki takriban kumi ,bendi hiyo pia imezungukwa na
wataalamu .
Ngoma
Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi mengi ya utani au
usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina
ambayo bendi hiyo haiwezi kuyakwepa ! Jina lingine ambalo lilikua gumu
kwao kulikubali ni “Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na
baadhi ya wadau wa mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa vitisho vya mbwa
wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !
NGOMA AFRICA BAND NA MZIMU WAO WA MZIKI WA DANSI ! WENYE MVUTO MKUBWA BARANI ULAYA
Reviewed by crispaseve
on
04:00
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
04:00
Rating:

Post a Comment