CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D’OR KWA MARA YA TATU
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano
Ronaldo, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maarufu kama FIFA
Ballon D’or kwa mara ya tatu katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi
wa Kongresshaus mjini Zurich, nchini Uswisi.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 29, ameifungia timu yake ya
Madrid inayoshiriki ligi kuu ya Hispania ‘La Liga’ jumla ya mabao 31
katika michezo 30 ambayo alicheza katika msimu huu na kuwagalagaza
wapinzani wake ambao ni Straika wa barca, Lionel Messi na kipa ‘Manuel
Neuer’ anayeidaikia klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuibuka mshindi wa Tuzo hiyo kwa kupata Kura asilimia 37.66, Messi 15.76 na Neuer kura 15.72.
”Pindi unaposubiria kusikia jina likitajwa, ni wakati mgumu”, alisema Ronaldo na kuongeza, ”Najua
ni kiasi gani bidii ya kazi na jitihada ambazo zimenifanya nishinde
tuzo hii, na ndio maana bado napatwa na hisia, haijalishi ni mara ngapi
nimekuja hapa kuipokea, natumaini nitafanya hivyo kwa miaka mingi
ijayo”.
Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno
kuchukua Tuzo hizo mara nyingi ikiwa ni mara yake ya tatu baada ya
kufanya hivyo mwaka 2008 na 2013
Pia Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu
barani Ulaya baada ya kufunga jumla ya magoli 17 katika michuano hiyo
msimu wa 2013/14.
Katika Tuzo hizo, Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew ameweza
kuibuka na tuzo ya kocha bora wa mwaka, Mshambuliaji wa Colombia ‘James
Rodriguez’ akitwaa Tuzo ya goli bora la mwaka, Mwanadada Nadine Kessler
anayechezea timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani akitwaa tuzo ya
mchezaji bora wa kike, Ralf Kellerman akinyakua tuzo ya kocha bora wa
timu ya wanawake pamoja na Hiroshi Kagawa akishinda tuzo ya urais bora
wa mpira wa miguu.

Cristiano Ronaldo na mchumba wake Irina Shayk baada ya kuwasili katika sherehe za utoaji tuzo za Ballon D’or

Messi na kifaa chake Antonella

James Rodriguez na kifaa chake

Lionel Messi akiwasainia mashabiki wake

Kipa wa Ujerumani na Bayern, Neuer akiwasaini mashabiki

Ronaldo na Marta wakipata uselfie

Cristiano Ronaldo na Nadine Kessler wakipata ukodaki

Rais wa shirikisho la FIFA, Sepp Blater akimpingeza Ronaldo kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia

Ronaldo akishangilia baada ya kutangazwa mshindi

Ronaldo akiwa amebeba Tuzo yake ya chezaji bora wa Dunia

Straika wa Colombia, James Rodriguez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya goli bora la mwaka

Cristiano Ronaldo akimkabidhi kijana wake Ronaldo Jr Tuzo yake

Joachim Low akisema machache baada ya kukabidhiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka

Kikosi cha timu ya Dunia wakipata ukodaki
CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D’OR KWA MARA YA TATU
Reviewed by crispaseve
on
00:01
Rating:


Post a Comment