MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD
Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua
jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar.
Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald
Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha
Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Andrew Chale
KAMPUNI
ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo
imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa
mara ya kwanza hapa Nchini. Akizungumza na wandishi wa habari mapema
leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania,
Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi
hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora
mzuri zaidi.
Pia
alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi
pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1. “Wateja wa DStv
watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa
kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania”
alisema Ronald Shelukindo.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora
wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa
habari leo jijini Dar.
Ronald
Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia
vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa
kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.
King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani
ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi
akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda
umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua
Ronald Shelukindo.
Kwa
upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu
aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD,
ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei
rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa
wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka
kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha
king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
“Ofa
hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo
michuano hii itakapofikia tamati ambapo bei itabadilika kutoka hizi za
sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara ya
kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.”
Alisema Furaha Samalu.
Kwa
upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi
alieleza kuwa, siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele
kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa
digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.
“Huduma za DStv siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta
usumbufu. Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na
hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo... Hivyo ni
wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.
Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za
king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya
Tsh. 99,000/ kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za
michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa
gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya
DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.
Katika
hatua nyingine, DStv wamezindua huduma mpya kwa wateja wao
waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia
huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’,
Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa
kupokea usajili wa ‘App’.
Akielezea,
juu ya huduma hiyo, Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa
ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na
kisha kujisajili kupitia ‘App’ kwa kujisajili kwa kuandika ‘DStv
Now’.
Aidha,
Ronald Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa
wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma
hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya
Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.
Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma
mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia
simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet.
Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving'amuzi vya DStv
kupitia akaunti zao.
Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia
promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now "application"
inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato
(Laptop) unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na
king'amuzi kipya cha DStv HD.
MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD
Reviewed by crispaseve
on
11:20
Rating:
Post a Comment