PICHA:RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK ALIPOWASILI NCHINI JANA USIKU
Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akishuka kwenye ndege akiambatana na
mkewe Bi. Schadt wakati
akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jana usiku jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akiwa
mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh.
Joachim Gauck na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.
Mohammed Gharib Bilal
wakifurahia jambo walipokuwa wakitazama vikundi
mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya
Rais huyo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana
usiku jijini Dar es salaam.
Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akiwa na mkewe Bi. Schadt na Makamu wa
Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi
mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa
Ujerumani
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana usiku jijini Dar es
salaam.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa
Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha. Picha na Aron
Msigwa - MAELEZO.
----
Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na msafara wake amewasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa
2.40.
PICHA:RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK ALIPOWASILI NCHINI JANA USIKU
Reviewed by crispaseve
on
07:35
Rating:
Post a Comment