Dkt Mwele: Kutoka binti mwenye ndoto kuwa mtafiti hadi mwanasayansi wa kimataifa hadi muwania Urais2015
Mapema
wiki hii, mwanasanyansi wa kimataifa Mtanzania, mwanamama Dokta
Mwelecele (Mwele) Malecela, alitangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania
kwa kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM. Dokta Mwele
ambaye hadi wakati anatangaza uamuzi huo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ana historia ya kipekee ambayo
nilibahatika kuifahamu kupitia chapisho moja lililopo katika blogu hii.
Hata hivyo, chapisho hilo ambalo lilisomwa na maelfu ya watu, lilikuwa
katika lugha ya Kiingereza. Makala hii ni marudio ya chapisho hilo kwa
lugha ya Kiswahili. Maelezo hayo yanatoka mdomoni mwa Dkt Mwele mwenyewe
ila mie nimetafsiri tu kwa Kiswahili.
Ajira yangu katika
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni hadithi ya bahati yenye
matokeo mazuri ambayo awali haikuwa katika nia yangu. Nilijiunga na taasisi
hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya
wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, nilipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani
(Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian
Filariasis.
Nilishawahi kusikia kuhusu ugonjwa huo nilipokuwa mwanafunzi UDSM
chini ya uangalizi mzuri wa Mhadhiri Dokta Parkin lakini sikujua nini nitafanya
kuhusiana na ugonjwa huo. Kichwani mwangu, nilitamani kufanya kazi kuhusu
ugonjwa wa malaria ambao kwa wakati huo nilidhani ulikuwa eneo la kuvutia
kiutafiti. Kwahiyo, lazima Nikiri kwamba nilifadhaika kujikuta nashughulikia
ugonjwa wa Bancroftian Filariasis badala ya malaria, ambayo ilikuwa na nyenzo
nyingi kwa maana ya vifaa na ufadhili. Hata hivyo, niliambiwa bayana kuwa
lazima nishughulikie kufufua shughuli ya ugonjwa huo wa Bancroftian Filariasis
hapo Amani.
Nikiwa mtu ninayependa
kukabiliana na changamoto, nikaanza safari ndefu ya kupita Milima ya Usambara,
kuelekea sehemu hiyo inayoitwa
Amani.Safari ilikuwa katika mlolongo wa kupanda na kushika vilima kama mawimbi
vile hadi wakati flani sikuona watu wala makazi. Hofu yangu ilipunguzwa na
mandhari mazuri, misitu ya kupendeza, na hewa ilivyokuwa mwanana kadri
tulivyopanda milima.
Dkt Mwele: Kutoka binti mwenye ndoto kuwa mtafiti hadi mwanasayansi wa kimataifa hadi muwania Urais2015
Reviewed by crispaseve
on
10:28
Rating:
Post a Comment