MIILI YOTE 23 YA AJALI YA BASI LA ANOTHER G NA LORI MUFINDI IRINGA YATAMBULIWA , DC MBONI AWAPA USHAURI TBS KUKAGUA UBORA WA VYOMBO VYA USAFIRI
Mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita kushoto akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo ya Mufindi katika kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi |
Baadhi ya ndugu wakichukua mwili wa ndugu yao baada ya kuutambua |
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)
akimfariji mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya basi la Another G na
lori iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana ,wengine pichani ni wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mufindi (picha na matukiodaimaBlog)
Na MatukiodaimaBlog.
MIILI yote 23 ya ajali ya basi aina Coster mali
ya kampuni ya Another G lenye namba
za usajili T 927 CEF aina ya mitsubishi fuso iliyokuw3a ikifanya safari
zake kati ya Iringa – Njombe ambalo liligoganga na uso kwa
uso na lori lenye namba za
usajili T 916AQM likiwa na Tela lenye namba za usajili T 965 BEH
Scania imetambuliwa na ndugu zao.
Kwa
mujibu wa mkuu wa wilaya ya Mufindi ambae ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya Bi Mboni Mhita kuwa ndugu wa
marehemu hao waliokufa katika ajali waliweza kutambua miili ya
ndugu zao jana na leo na kuwa hadi sasa hakuna mwili ambao bado
kutambulia na hivyo kuvishukuru vyombo vya habari kwa kushiriki
kuhabarisha juu ya ajali hiyo na wananchi ambao waliitikia na
kufika kutambua miili hiyo .
MIILI YOTE 23 YA AJALI YA BASI LA ANOTHER G NA LORI MUFINDI IRINGA YATAMBULIWA , DC MBONI AWAPA USHAURI TBS KUKAGUA UBORA WA VYOMBO VYA USAFIRI
Reviewed by crispaseve
on
11:37
Rating:
Post a Comment