SHEIKH SHARIFU MSOPA ATOA OFA YA MAOMBI KWA VIONGOZI NA WANANCHI KUTUMIA MAFUTA MAALUMU TOKA GUBA YA UAJEMI KUWAPAKA
Sheikh
Sharifu Msopa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari Dar es
Salaam leo Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo
maalumu.
Sheikh
Sharifu Msopa (kulia), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo
Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo maalumu. Kshoto ni
Sheikh Maulana Salim.
Sheikh Maulana Salim (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na bloggers
wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SHEIKH
Sharifu Msopa ametoa ofa kwa viongozi na wananchi nchi nzima ya
kuwafanyia maombi pamoja na kuwapaka mafuta maalumu ya uponyaji kutoka
Guba ya Uajemi.
Sharifu
Msopa ametoa ofa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, ambapo alisema walengwa zaidi ni watu maskini, viongozi
mbalimbali wale waliotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali kuelekea
uchaguzi mkuu.
Alisema
lengo la maombi hayo ambayo hayachagui dini ni kuwapata viongozi
waliochaguliwa na mungu ambao wataliongoza taifa wakiwa na hofu ya
mungu.
"Maombi
tutakayofanya hayambagui mtu na dini yake kwani tumekuwa tukitoa huduma
hii ya maombi bure kwa kushiriana na wenzetu wa kristo na tayari baadhi
ya viongozi tumeanza kuwafanyia maombi na yule aliyetayari awasiliane
nasi" alisema Sharifu Msopa.
Msopa
alisema suala hilo la imani ni muhimu sana hasa katika kipindi hichi cha
kuelekea uchaguzi mkuu na kuwa lengo kubwa ni kuona nchi inapata
viongozi waliobora na si bora viongozi kupitia maombi yao.
Alisema
baada ya kufanyiwa maombi mtu husika atapakwa mafuta ya ajabu kutoka
Guba ya Uajemi ambayo yananguvu ya kuondoa mikosi, uchawi na kumletea
bahati muombewaji.
Alisema
hivi sasa wapo katika maombi ya mwezi mzima ya kuwaombea, viongozi wa
siasa serikali, wafanyabiashara, maskini na makundi mengine ili wapate
neema hiyo.
Msopa
alisema anaamini kuwa kupitia maombi kiongozi mzuri atapatikana kuanzia
ngazi ya udiwani, ubunge na urais na kuwa mara baada ya mtu husika
kupakwa mafuta hayo kama atakuwa na uchawi, nuksi na mambo mengine
yatamtoka kwa njia ya kuharisha, kutapika na kumfanya awe huru.
Alisema maombi hayo anatarajia kuyafanya nchi nzima kwa kukutana na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi.
Alisema
kwamba maombi kama hayo amekuwa akiyafanya katika nchi mbalimbali
duniani na yamewasaidia watu wengi kutoka dini zote za kikrito na
waislamu na amekuwa akiyafanya bure. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
SHEIKH SHARIFU MSOPA ATOA OFA YA MAOMBI KWA VIONGOZI NA WANANCHI KUTUMIA MAFUTA MAALUMU TOKA GUBA YA UAJEMI KUWAPAKA
Reviewed by crispaseve
on
10:16
Rating:
Post a Comment