SULEIMAN NYAMBUI AWAAGA WATANZANIA AKISONONEKA
Katibu
Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui
(kulia) akikabidhiwa suti ya michezo yenye bendera ya Tanzania kutoka
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally atakazozitumia
wakati akifubndisha riadha nchini Bunei barani Asia ambako amepata
mkataba wa kufundisha riadha kwa miaka miwili. (Picha na Peter Mwenda).
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports,Abbas Ally akimkabidhi zawadi ya suti
Katibu Mkuu wa zanmani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suliman
Nyambui anayekwenda kufanya kazi ya kufundisha riadha nchini Bunei,Asia.
KATIBU
Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) aliyeachia wadhifa huo,
Suleiman Nyambui ameiasa Serikali kuwa ikitaka kurudisha heshima ya
michezo kama zamani ni lazima irudishe vipindi vya michezo (Physical
Education PE) kuanzia shule za msingi.
Nyambui
ambaye amejing’atua kuendelea na madaraka yake ya Ukatibu Mkuu wa RT
baada ya kuingia mkataba wa kufundisha riadha kwa kipindi cha miaka
miwili nchini Brunei barani Asia, alisema Tanzania kama haitarudisha
michezo katika programu zake hakutakuwa na ushindi.
Alisema
Serikali ikiweka mikakati ya michezo na kutenga viwanja vyenye ubora
vya kuchezea tutaendelea kuwa wasindikizaji katika michezo yote ya
riadha, soka, netiboli, ngumi na mingine ambayo kila wachezaji
wakishiriki hakuna ushindi unaopatikana kulinganisha na zamani ambako
wao waliwika.
Nyambui
alisema Tanzania imejaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji na baadhi ya
maeneo yanayofaa kwa ajili ya kujenga viwanja na kuweka kambi za mazoezi
kwa timu za taifa kama Tanga,Mbulu, Arusha, Singida, Njombe, Makambako
na Mbeya ambako hali ya hewa inaruhusu wachezaji kufanya mazoezi kwa
nguvu.
Alisema
kutofanyika mashindano ya michezo katika ngazi za wilaya inawanyima
wachezaji wengi wenye vipaji kuonesha uwezo wao wa kujituma kutumikia
taifa katika michezo kwa sababu hawaonekani.
Akipokea
zawadi ya suti na vifaa vya michezo vyenye bendera ya Taifa kutoka
Kampuni ya Isere Sports, Nyambui alisema Serikali pia inatakiwa
kuwasaidia waagizaji na wauzaji wa vifaa vya michezo wapunguziwe ushuru
ili wauze vifaa hivyo kwa bei nafuu.
Nyambui
aliyewahi kuwa mshauri wa ununuzi wa vifaa vya michezo wa Kampuni ya
Isere alisema katika kipindi cha miaka miwili atakayokuwa nje ya
Tanzania bado ataendelea kutoa ushauri kwa watanzania wa njia nzuri ya
kujikwamua.
SULEIMAN NYAMBUI AWAAGA WATANZANIA AKISONONEKA
Reviewed by crispaseve
on
09:47
Rating:
Post a Comment