UMITASHUMTA changamoto
Meneja mauzo wa Isere Sports, Rasul Ndee akionesha aina ya mipira inayofaa kuchezewa katikaviwanja mbalimbali hapa nchini
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere, Abbas Ally akionesha ainaya viatu vinavyofaa katika viwanja mbalimbali nchini
MASHINDANO ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za Msingi Tanzania
(UMITASHUMTA) umemalizika mjini Mwanza huku ikiacha changamoto kwa
Serikali kushirikisha wadau kufufua na kuendeleza vipaji.
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally ambao ni wauzaji wa
vifaa michezo nchini aliyekuwa shuhuda wa michezo hiyo Mwanza alisema
Tanzania imejaa vijana wenye vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa.
Alisema mikoa mingi imetia fora katika michezo hiyo ikiwemo mkoa wa
Manyara,Singida na Mara ambako kujitokeza vijana wengi kupenda mchezo wa
riadha na walifanya vizuri katika michezo hiyo.
Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally
alisema mikoa mingi ilijiandaa kwa mashindano hayo lakini kuna tatizo la
waamuzi ambao walionesha upendeleo kwa timu za Kanda ya Ziwa.
Alkisema mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa
medali 26 ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka baada ya kupachikwa
bao 1-0 na wenyeji Mwanza.
Ofisa Michezo Mkoa wa Morogoro, Neema Msita alisema kama vipaji
vilivyoneshwa katika michezo ya mwaka huu vitaendelezwa Tanzania
itarudisha heshima katika michezo kimataifa.
Alisema alitoa witokwa klabu zote kuanzisha timu za watotoambazozitalea
vipaji kutokahatuaya shule za msingi, Sekondari na Vyuoni kwa vile
Tanzania imejaliwakuwa na vipaji katika michezo yote.
Mtangazaji
wa TBC Taifa, Jesse John aliyeshuhudiaufungaji wa mashindanohayo
alisema kama kauli ya Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa ya kuwa wizara
yake itasaidiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kusimamia
ukuzaji wa elimu sambamba na michezo utafanyiwa kazi hakuna timu ya
taifa yaTanzania itakayotolewa katika mashindano kirahisi.
UMITASHUMTA changamoto
Reviewed by crispaseve
on
06:27
Rating:
Post a Comment