WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA
Pichani:
Baadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mawasilisho ya wanasayansi wenzao
yaliyokuwa yakiwasilishwa katika mkutani huo ulioanza Julai 7 na
kumalizika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi mkubwa wa makao makuu ya
UNESCO, Paris, Ufaransa.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris,
Ufaransa] Wanasayansi zaidi ya 2500, kutoka pembe zote duniani
wamekutana katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate
Change’.
Mkutano
huo ulioandaliwa katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa,
ulikuwa wa siku nne (Julai 7-10) na ndio ulikuwa mkutano mkubwa zaidi wa
wanasayansi duniani kuanda makataba ambao unatarajiwa kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi utakaofanywa hapo Desemba, mjini Paris.
Ushiriki
wa wanasayansi hao katika mkutano wao huo umefanya jiji la Paris kuwa
na pilikapilika za hapa na pale hasa viunga vya makao makuu ya UNESCO na
yalipokuwa yanafanyika matukio ya mkutano huo.
Miongoni
mwa mada zilizowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na namna ya
dunia itakavyokabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to
reduce temperature level by 2 degrees), mafuliko yanayokumba nchi
mbalimbali duniani (Floods). Mada zingine ni kama vile misitu, athari za
watu kuongezeka mijini, ongezeko la joto, kupungua kwa vina vya
bahari, masuala ya hewa ukaa, gesi sumu na mengine mengi yanayopelekea
athari za tabianchi.
Mkutano
huu ulilenga jinsi ya kukabiliana na tabianchi pamoja na kubadilishana
ujuzi zaidi hii ikiwa ni kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama
wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika hapa hapa Paris ,
Desemba mwaka huu.
Hata
hivyo matarajio ya wanasayansi wengi wakiwemo kutoka nchi tofauti
wameeleza kuwa, hadi kufikia mkutano wa COP 21, hiyo Desemba mataifa
yataafikiana maamuzi ya kila mmoja wapo pindi watakapo wasilisha.
WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA
Reviewed by crispaseve
on
02:34
Rating:
Post a Comment