BENKI YA CBA TANZANIA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE NCHINI
Baadhi
ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania, DK. Gift Shoko akiongea na wateja wa
benki hiyo (hawapo pichani) wahudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa
wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
4/5/12:Baadhi
ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo
katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Imam
Mkuu wa Masjid Ma, Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa mawaidha wakati
wa futari iliyoandaliwa na Benki ya CBA katika Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya wateja wake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CBA, Dk.Gift Shoko (wa nne kushoto) na Imam Mkuu wa
Masjid Ma, Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.
Yafuturisha
wateja wake Dar es Salaam. Benki ya CBA Tanzania imewafuturisha baadhi
ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuboresha
uhusiano na wateja ambapo pia itawaandalia wateja wake futari kwenye
maeneo mbalimbali yalipo matawi nchini. Akizungumza wakati wa futari
iliyoandaliwa na CBA Tanzania kwa wateja katika Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk.Gift Shoko alisema “
Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki
yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana
tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili
pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo
kwenye futari hii”.
Alisema
Benki ya CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake
katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata
katika matukio ya kuchangia kuinua sekta mbali mbali mfano afya na
elimu. “Lakini leo ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa
tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao
unaendelea”.
Dk.Shoko
aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake ili
ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni
huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata
huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.“Benki ya CBA Tanzania
tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi mema ya
sikukuu!, endeleeeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na msiache
kutembelea matawi yetu au kutembelea mtandao wetu kwa njia ya kisasa ya
kuona huduma zetu mbalimbali kama vile huduma ya mkopo wa bima ambayo
inaonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi,mikopo ya kununua nyumba yenye
masharti nafuu pia tunatoa huduma ya M-Pawa kwa kushirikiana na Vodacom
inayowezesha wateja wa M-Pesa kuweka akiba na kupata mikopo kwa haraka
na bila masharti magumu.”
Alisema
Benki ya CBA Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia
uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na
kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Bado CBA ina mpango wa kutoa
misaada katika mikoa mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza
tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu. CBA
Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na
Tanzania, CBA Tanzania ina matawi kumi na moja yaliyosambaa sehemu
mbalimbali nchini.
BENKI YA CBA TANZANIA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
07:06
Rating:
Post a Comment