TASAF YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Watumishi
wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kilele cha wiki ya
Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar Es
Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho
ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa
huduma kwa wananchi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga, ( hayupo pichani)
kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa
wananchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti)
akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi
(hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma
yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa
salaam.
Na Estom Sanga-TASAF.
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameadhimisha
wiki ya Utumishi wa Umma kwa Menejimenti ya taasisi hiyo kukutana nao
kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es
Salaam na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi ili
kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini
Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za
kupambana na Umaskini nchini..
Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza
kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi
wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo
wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na
kuongeza uchumi wao.
TASAF YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Reviewed by crispaseve
on
07:15
Rating:
Post a Comment