DC MBULU: AWAOMBA WANANCHI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI
Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga amewataka wananchi
wamuunge mkono Rais John Mafuguli, katika kuhakikisha anasimamia
rasilimali za watanzania na kufanikisha maendeleo ya sekta mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Mofuga, wakati inakaribia miaka miwili ya utawala wa Rais
Magufuli amefanikisha maendeleo mengi ambayo yangeweza kufanyika kwa
kipindi cha utawala wamuda wa miaka 40.
Akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Mbulu, alisema miongoni mwa maendeleo hayo ni
kuzindua na kuanza kwa ujenzi wa reli ya umeme, kuhamisha makao makuu ya
nchi Dodoma mpango uliodumu tangu mwaka 1973 na kuanza maandalizi ya
ujenzi wa barabara za ghorofa kwenye jiji la Dar es salaam.
Alisema
amefanikisha kuongezeka kwa pato la Taifa kupitia ukusanyaji wa kodi
kutoka sh850 bilioni kwa mwezi alipokuwa anaingia madarakani hadi
kufikia sh1.2 trilioni kwa mwezi hivi sasa.
Alisema
pia Rais Magufuli amefanikisha ununuzi wa ndege na kufufua shirika la
ndege la ATCL, kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari jambo
linaloongeza usajili wa wanafunzi mara mbili.
"Amegundua
watumishi wenye vyeti feki 9,932 na watumishi hewa 19,706 ambao
mishahara yao ilikuwa inatumiwa na watu wachache badala ya kupelekwa
kwenye shughuli za maendeleo za wananchi ikiwemo elimu, afya na maji,"
alisema Mofuga.
Alisema
Taifa lilishuhudia historia nyingine baada kupokea ripoti ya tume
aliyounda ya kuchunguza mchanga wenye dhahabu (makinikia) yenye wajumbe
nane wenye taaluma mbalimbali za uhandisi na kuchukua hatua stahiki mara
baada ya kupokea.
"Kwenye
taarifa hiyo ilibainika kuwa thamani ya madini yote kwenye makinikia ni
makontena 277 yenye thamani ya sh829.4 bilioni kwa viwango vya wastani
na viwango vya juu ni sh1.4 bilioni yaani dhahabu iliyokuwa kwenye
makontena 277 ni sawa na lori mbili za tani saba ba pick up tani 1.5,"
alisema Mofuga.
Alisema
Taifa lilikuwa linahitaji kiongozi aina ya Rais Magufuli kwa muda mrefu
na kutokana na utekelezaji huo unaofanyika wananchi wanatakiwa kumuunga
mkono ili aongeze jitihada za kuhakikisha Tanzania inafika kwenye nchi
ya maziwa na asali.
Mmoja
kati ya wakazi wa eneo hilo Yohana Amnaay alisema pamoja na jitihada
hizo za Rais Magufuli pia mkuu huyo wa wilaya ya Mbulu Mofuga, amekuwa
na utaratibu mzuri wa kutatua kero za jamii hasa migogoro ya ardhi kwa
kukutana na wananchi.
"Kila
alhamisi DC wetu amekuwa na utaratibu wa kukutana na wananchi hivyo
kupitia nafasi hiyo jamii imekuwa inatatuliwa kero zake kuliko kukaa na
kusubiri viongozi wakubwa wafike Mbulu ndiyo wananchi wafikishe
malalamiko yao kwao," alisema Amnaay.'
DC MBULU: AWAOMBA WANANCHI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI
Reviewed by crispaseve
on
04:21
Rating:
Post a Comment