MVUA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA MKURANGA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kutokana
na mvua zinazoendelea katika maeneo tofauti barabara mbili zimekata
mawasiliano na kufanya baadhi huduma za kijamii kushindwa kufanyika.
Barabara zilizokata mawasiliano ni barabara ya Chamanzi kwenda Kibamba pamoja na barabara ya barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
amesema kuwa hali ya barabara katika jimbo lake ziko katika hali mbaya
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Amesema
kuwa ameomba barabara ya Kimazichana kwenda Kibamba kuingizwa katika
barabara za Tanroads ili ziweze kuangaliwa kutokana umuhimu wake katika
uchumi wa nchi.
Diwani
wa Kata ya Tengerea , Shaban Manda amesema kuwa barabara ya Mkuranga
kwenda Hoyoyo makaravati yaliyowekwa hayawezi kuhimili mvua ikiwa kubwa.
Amesema
wakandarasi wanatakiwa kushirikisha wananchi katika uwekaji wa madaraja
na makaravati kutokana na wao ndio wanajua sehemu zenye matatizo.Manda
amesema kuwa wakati mwingine sehemu zinazowekwa makaravati hayana
umuhimu ndio maana mvua zikinyesha nayo yanakwenda na maji .
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kimazichana , Omary Ndeu amesema hali mbaya kwa wananchi
wa Mbezi na Kibamba hawawezi kufika kimazichana ambapo huduma za kijamii
na biashara ndio zinafanyika.
Wananchi
wakishuka katika daladala inayofanya safari zake Kibamba , Kimazichana
na Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kutokana na barabara hiyo kukatika
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Vijana
wakitengeneza barabara ya dharula kwa ajili ya kupitisha magari na
kupata kipato kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha zote na
Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo ikiwa imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda akizungumza na Michuzi Blog juu ya barabara hiyo kukatika na kukatika kwa mawasiliano.
MVUA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA MKURANGA
Reviewed by crispaseve
on
10:55
Rating:
Post a Comment