MAJALIWA ATOA MSAADA WA BAISKELI 40 KWA WALEMAVU
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa akimsukuma kwenye baiskeli Nasim Mohamed baada ya kukabidhi msaada wa baikeli 40 kwa walemavu katika hafla iliyofanyika Kata ya Mandawa, Ruangwa, mkoan Lindi hivi karibuni.
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [TAMISEMI], anayeshughulikia Elimu, Kassm Majaliwa ametoa msaada wa baiskeli 40 kwa ajili ya kusaidia watu mbalimbali wenye ulemavu katika wilaya ya Ruangwa.
Pia alitoa baiskeli tano kwa ajili ya kubebea wagonjwa wasioweza kutembea katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa pamoja kukabidhi shuka 100 zilizotolewa na NHIF kwa ajili ya hospitali hiyo.
Wakati akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Majaliwa alisema kuwa suala la kusaidia walemavu ni jukumu la kila mtu hivyo wananchi hawanabudi kushirikiana na kuwasaidia kwa hali na mali ili nao waweze kufanikisha kupata mahitaji yao.
Majaliwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa alisema kuwa baiskeli hizo zitawasaidia kwa kuwawezesha kwenda shule na sehemu yoyote kwa urahisi tofauti na awali ambapo walikuwa wanashindwa kutokana na hali zao.
Alisema kwa kutumia baiskeli hiyo mzazi ambaye alikuwa anambeba mtoto wake mlemavu na kumpeleka shule, hospitali na kwingineko sasa atakuwa amerahisishiwa kwani baada ya kubapa baikeli hizo wanaweza kutembea wenyewe kwa kujiendesha hivyo kuwapungua mzigo wazazi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Hamidu Masare alimshukuru mbunge kwa kuwapatia shuka 100 pamoja na viti vitano ambapo alisema vitu hivyo vilikuja wakati muafa kwani wanauhaba mkubwa wa mashuka hadi kusababisha baadhi ya wagonjwa kutandika vitenge vyao katika vitanda vya hospitali.
Issa Libaba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, alitumia fursa hiyo kumpongeza Majaliwa kutokana na jitihada mbalimbali anazozifanya kwa ajili ya kusaidia wananchi pamoja na maendeleo ya wilaya kwa ujumla.
Baadhi ya wazazi ambao wana watoto walemavu ambao walipatiwa msaada wa baisketi hiyo walimshukuru Majaliwa kwani wao walishindwa kuwanunulia watoto wao baiskeli hizo kutokana na kipato chao kuwa duni.
"Sasa naweza kupumzika na kufanya shughuli zangu kwa ufasaha kwani nilikuwa nashindwa kwa sababu muda wote nililazimika kumbeba mtoto wangu mgongoni kutokana na iulemavu alikuwa nao, sasa naweza kumuweka katika kiti chake na kuendelea kazi zangu vizuri pia naweza kwenda naye popote kwa kutumia baiskeli, sina zaidi ya kumshukuru mbunge," alisema Marco Fidel baada ya kukabidhiwa baiskeli ya mtoto wake mwenye ulemavu wa miguu na mikono.

Post a Comment