KINANA AITEKA WILAYA YA HANANG,AIBOMOA CHADEMA MKOANI MANYARA,
Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akimhoji kwa kifupi Mwenyekiti
wa Chadema wa Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba alikopeleka hati ya
mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto
ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo
haijulikani nani analipwa nani na uko wapi..
Hatua
hiyo ya kumhoji ilifikiwa baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye
mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto, kuwa
viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la
soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya
kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini
alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo,
jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka
wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba ili
serikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo.
Katibu wa NEC Itakadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hanang,Bwa.Augustino Mayumba mara baada ya kujibu tuhuma mbele ya Wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,akidaiwa kuficha mkataba wa
mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao
alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani
nani analipwa na uko wapi..
Katibu
Mkuu wa CCM,akipeana mkono na Katibu Kata wa CHADEMA,waka Kata ya
Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas mara baada ya kukabidhi kadi yake
cha chama hicho na kujiunga na chama cha CCM
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na wafuasi wakuu wa CHADEMA,walioamua
kujiunga na chama chama CCM baada ya kuzikabidhi kadi zao kwa Ndugu
Kinana.Kulia ni Meshack Kim,Katibu Kata wa CHADEMA,waka Kata ya
Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas na mwisho kusho ni Elisante Taulo
Aliyewahi
kuwa mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick
Sumaye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Gendabi kata ya
Gendabi,Wilayani Hanang mkoani Manyara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipokuwa kwenye ziara mkoani humo.
Baadhi
ya Akina Mama wa kijiji cha Gendabi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye mkutano wa hadhara wa katibu Mkuu,wilayani Hanang mkoani Manyara.
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akizungumza jambo na Mbunge
wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu walipokuwa kwenye mkutano wa hadhara
katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi wilayani Hanang mkoani
Manyara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia baadhi ya wananchi wa kijiji cha
Gendabi kata ya Gendabi,Wilayani Hanang mkoani Manyara
Wananchi
wa kijiji cha Barjomot wakishangilia jambo wakati katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia na kuweka jiwe la msingi kwenye
ofisi ya CCM,Wilayani Hananga mkoani Manyara.
Ndugu
Kinana akiwahutubia baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Barjomot mara baada
kuweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya CCM,Wilayani Hananga mkoani
Manyara.
Kinana akishiriki kusomba mawe kwa ajili ya kujengea sakafu jengo la CCM katika Kata ya Qaloda, wilayani Hanang
Kinana
akipiga mpira kufunga bao ikiwa ni ishara uzinduzi wa michuano ya soka
kwa vijana Endasak, wilayani Hanang, ambapo Mbunge wa Jimbo la Hanang,
Dk. Mary Nagu alizizawadia timu zitakazoshiriki mipira na jezi.
Katibu
wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akipokea mabango yenye jumbe
mbalimbali yaliokuwa yamebebwa na wananchi,katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Endasak,Wilayani Hanang mkoani Manyara,pamoja na hayo Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alitoa majibu kwa wananchi hao na kuonesha
kuridhika nayo.
Wananchi
wa Endasak wakimsikiliza katibu Mkuu,Ndugu Kinana alipowahutubia na
kujibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha kwa njia mabango
Kinana akuhutubia Wananchi katika Kajiji cha Endasak wilayani Hananga mkoani Manyara.Kinana
ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye
ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Wasichana wa kabla la Wabarbaig wakishiriki katika mapokezi ya Kinana katika Kijiji cha Mwahu, Hanang
Katibu
wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM,mjini
Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara
Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM,mjini Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
CCM,mjini Katesh,wilayani Hanang mkoani Manyara.Ndugu Kinana
ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa
kwenye ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi
ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia
ufumbuzi.
Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, katika mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, wakati
Kinana alipowasili katika Wilaya ya Hanang, akitokea mkoani Singida,
kwenda kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza
kero za wananchi na njia ya kuzitatua katika mkoa wa Manyara
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme wakati wa mapokezi hayo.
Katibu
wa NEC-Itikadi,Siasa na Uenezi Nnape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa
jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu mara baada ya kupokelewa wilyani humo
mpakani mwa Singida na Hanang.
KINANA AITEKA WILAYA YA HANANG,AIBOMOA CHADEMA MKOANI MANYARA,
Reviewed by crispaseve
on
01:18
Rating:
Post a Comment