MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI VYA MCHEZO WA NGUMI KUFANYIKA JUNE 15
MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika June 15 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class atakaezichapa na Twalibu, Mussa Sunga atazidunda na Ally Muhulo,Charo Issa na Shabani Kaoneka,Dickson Tembo na Raymon Mbwango na Yakubu Abdallahman, Hassan Mijugu ataoneshana kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus.
Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidia mashindano hayo kwa namna moja au nyingine anaweza kuwasiliana na kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au unaweza fika katika klabu ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza kuwasiliana na kocha Super D
Reviewed by crispaseve
on
03:27
Rating:

Post a Comment