| Wajumbe wakifuatilia taarifa ya kamati kwa umakini.
Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa waendelea na vikao ambavyo vinafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dodoma.
Vikao hivyo ambavyo vilianza rasmi tarehe moja June 1, 2012. Vinaendelea leo hii hapa Dodoma, ambapo hoja mbalimbali zimekuwa zikijadiliwa kwa kina, ambapo vikao vilivyotangulia vimejadili juu ya hoja ya Katiba Mpya na suala la Muungano wa Serikali ya Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania. Ambapo wajumbe walichangia hoja mbalimbali za msingi kwa kuzingatia hali ya sasa ya siasa nchini na matukio sambamba na hoja hiyo, kama vile mijadala ndani ya majukwaa mbalimbali juu ya muundo wa Katiba ya sasa, mapungufu yake na mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya na pia mijadala juu ya maboresho ya Muungano.
Pamoja na hayo, kikao kinachoendelea hivi leo,kitajadili juu ya mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha na kuboresho Umoja huo wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mapendekezo hayo juu ya jinsi ya kuboresho umoja huo yametolewa na Kamati maalum ambayo ilipewa jukumu la kupendekeza namna ya kuiboresha UVCCM katika kikao cha Baraza hili kilichokaliwa mnamo tarehe 19/03/2011, ili iweze kukidhi mahitaji ya Siasa za ushindani wa sasa na baadae. |
Post a Comment