MATUKIO KATIKA PICHA MAZISHI YA MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA AGNES YAMO
Baadhia ya waombolezaji wakiwa
wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti
la Tanzania Daima, marehemu Agnes Yamo, tayari kwa ibada fupi ya
mazishi, nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogor jana mchana.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa
heshima za mwisho mwa marehemu Agnes Yamo, kabla ya mazishi yake, yaliyofanyika
kwenye makaburi ya Kola, mjini Morogoro jana mchana.
Ndugu, jamaa na marafiki
wakishusha kaburini jeneza lenye mwili wa marehemu Agnes Yamo, wakati wa
mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini Morogoro jana mchana.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya
Free Media Limited, Absalom Kibanda akiweka mchanga kwenye kaburi la merehemu Agnes Yamo,
wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini Morgoror jana mchana.
Baadhi ya
wafanyakazi wa Kampuni
ya Free Media Limited, inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na
Sayari,
wakiongozwa na Mhariri Mtendaji, Absalom Kibanda, wakiweka kwa pamoja
shada la maua katika kaburi la
marehemu Agnes Yamo. Agnes aliyekuwa mwandishi wa magazeti hayo,
amezikwa jana mchana kwenye makaburi ya Kola, Kigurunyembe mjini
Morogoro.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Frederick Werema akiweka shada la maua
kwenye kaburi la marehemu Agnes Yamo, baada ya kuzikwa katika makaburi ya Kola
mjini Morogoro jana mchana.
Mwanasheria Mkuu wa serikali,
Frederick Werema akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Agnes Yamo, kabla ya
mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola mjini Morogoro jana mchana.Picha zote na Joseph Senga
Reviewed by crispaseve
on
12:03
Rating:
Post a Comment