SERENGETI FIESTA 2012 NDANI YA LEADERS USIKU HUU
Sehemu
ya umati watu waliojitokeza kila kona jiji la Dar na kwingineko
kuwashuhudia wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la
Serengeti Fiesta 2012,akiwemo Mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini
Marekani,Rick Ross.
Wasanii wa kundi la
Wanaume TMK,likiongozwa na Mh Themba sambamba na Chege Chigunda
wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti
Fiesta 2012,linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar.uwanja wa Lidaz Club hapatoshi kabisa usiku
huu.
Nyomi la Watu ile balaa usiku huu.
Wasanii wa kikundi cha Makomando kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaa.
Msanii wa muziki wa
kizazi kipya Dyana pichani akionesha mbwembewe zake kabla ya kukamata
kipaza sauti,mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi usiku huu
ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
Msaniii mahiri wa kizazi kipya,Barnaba Boya kiimba jukwaani huku Dyana na skwadi lake wakionesha mbwembwe zao kama kawa.
Mmoja wa wshindi wa
shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Youk Killer akishusha mistari yake
nguvi usiku huu,huku shangwe na vigele vigele vikiwa vimetawala.
Mashabiki wakishangweka usiku huu vilivyo.
Mmoja wa washindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akifloo jukwaani. .
Baadhi ya mashabiki wakijiachia vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012
![]() |
| Mmoja wa wshindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,NeyLee akiimba jukwaani . |
Baadhi ya wasanii
kutoka nyumba ya vipaji THT wakiamsha amsha usiku huu wakati tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 likiendelea huku mashabiki na wapenzi wa tamasha
hilo wakiendelea kumiminika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz
Club,jijini Dar.
Mmoja wa wasanii
chipukizi kutoka kwa THT,akiimba kwa hisia mbele ya umati mkubwa wa watu
(haupo pichani),uliojitokeza kushuhudia wasanii wa hapa nyumbani na nje
wakitumbuiza katika jukwaa moja usiku huu.
Mmoja wa wasanii chipukizi akinogesha jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu
The Wacko Jako wa bongo akifanya vitu vyake jukwaani usiku huu
Baadhi ya wakazi wa
jiji la Dar na vitongoji vyake wakiwa tayari ndani ya viwanja vya Lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti
Fiesta likiendelea kurindima,huku wakimsubiri kwa hamu mwanamuziki wa
Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross ambaye anatarajia kukamua
usikuu huu.
Reviewed by crispaseve
on
02:44
Rating:





























Post a Comment