MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AZINDUA JUKUMU LA USAFIRISHAJI MAHABUSU KUTOKA GEREZANI KWENDA MAHAKAMANI NA KURUDI,MKOANI WA DODOMA
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi
jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na
kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa
Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambao walikuwa katika
uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali baada ya uzinduzi wa mabasi
mawili na gari ndogo moja (pick-up). Kushoto Mkurugenzi wa Mashitaka
nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza
Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha
moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia
Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa
wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi
mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia
mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa
Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza
wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika
katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Magari matatu ya kuwasafirisha
Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna
Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu Isanga Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.

Post a Comment