MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MZEE ALLY SYKES JIJINI DAR LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika
kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika
kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi.
Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na baadhi ya
wazee waliohudhuria shughuli za msiba, wakati alipokuwa akiondoka baada
ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini
Nairobi. Marehemu Sykes anatarajiwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es
Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa
marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa
mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes
anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
Reviewed by crispaseve
on
11:58
Rating:


Post a Comment