MBUNGE MSIGWA NA WENZAKE 70 WAACHIWA KWA DHAMANA
Na Francis Godwin wa Matukio Daima Blog,Iringa
SAKATA la vurugu za machinga na
polisi mjini Iringa limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi
mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mbunge wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine zaidi ya 70
Huku mahakama hiyo ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa watuhumiwa hao na kuwaonya kutofanya kosa kwa kipindi chote cha kesi hiyo inapoendelea kusikilizwa .
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya leo majira ya saa 8 mchana huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara wa magari zaidi ya matatu likiwemo gari ya maji ya kuwasha .
Mbali ya mbunge Msigwa kupanda
gari ndogo ya wazi ya polisi pamoja na watuhumiwa wawili wanawake
waliokamatwa katika vurugu hizo bado watuhumiwa wengine zaidi ya 70
walitumia usafiri wa karandinga la polisi.
Mbele ya mahakama hiyo wakili
wa serikali Adolph Maganda alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja
wanatuhumiwa kwa makosa matatu likiwemo la kushiriki mkutano na
kufanya vurugu ,uchochezi na kuharibu mali kinyume na sheria .
Huku mbunge akisomewa mashitaka mawili likiwemo kushawishi na kufanya mkutano bila kibali .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa hana pingamizi na dhamana kwa watuhumiwa hao wote ,hata hivyo wote wamekana mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa hana pingamizi na dhamana kwa watuhumiwa hao wote ,hata hivyo wote wamekana mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao.
Hata hivyo makimu anayesikiliza
kesi hiyo alisema kuwa dhamana kwa washitakiwa wote ipo wazi kwa
kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya
dhamana ya Tsh milioni moja .
Hadi majira ya saa 10 jioni
mahakama hiyo ilikuwa ikiendelea na mchakato wa kupitia barua za
dhamana kwa wadhamini huku mbunge akiwa wa kwanza kudhaminiwa ,mbali
ya mbunge watuhumiwa kati ya 74 waliokuwa bado kupata wadhamnini
ni watuhumiwa sita pekee.
Katibu wa chama cha Demokrasia
na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima
alisema kuwa mchakato wa kuwadhamini watuhumiwa wote waliosalia
unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa watuhumiwa wote
kudhaminiwa .
Hadi majira haya ya saa 10 .40
jioni wakati habari hii inakwenda mitamboni bado mahakama ilikuwa
ikiendelea na umati wa wafuasi wa Chadema ukiwa nje ya mahakama hiyo
kusubiri watuhumiwa hao kudhaminiwa .
Wakati huo huo wananachi
waliofika mahakamani hapo kushuhudia mbunge wao akifikishwa
mahakamani wamempongeza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa
Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka kwa kusimamia amani na utulivu katika
eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza kupambana na
machinga pasipo kumwaga damu kwa siku ya jana wakati wa vurugu hizo

Post a Comment