Miundo Mbinu mibovu ya dampo la Pugu Kinyamwezi yakwamisha zoezi la uzoaji taka baada ya magari ya taka kukwama kwa siku tatu.
Picha juu na chini ni Foleni ya
magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama katika dampo la Pugu
Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na ubovu wa miundo mbinu
huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo na kusababisha harufu
mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.(Picha na Dewji Blog).
Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
Masela wakifurahia baada ya gari
la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo
hilo kuelekea kumwaga taka.
Wanafunzi wa shule ya msingi
walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa
eneo hilo wakati wa saa za shule.
Wakazi wa maeneo hayo
wakichambua takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji na mifuko ya
plastiki ikiwa ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha maisha yao
ya kila siku, shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha kwamba chupa
wanazookota huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu kinachowapelekea
wafanyaji wa biashara hii kuwa watumwa wa pombe za kienyeji haswa
almaarufu kama Gongo au Chang'aa.
Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????
Magari ya Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo hilo, pichani
yakielekea kuwamga taka hizo baada ya barabara kutengemaa kwa kiasi.
Pichani ni juu na chini Mama
lishe wakitoa huduma ya chakula chini ya mti katika eneo lilizongukwa na
taka ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka hapa na pale lakini
vibarua wa dampo hilo hawana la kufanya.
Moja ya Katapila lililokodiwa na
Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam likiwa limekufa na kushindwa
kufanya kazi kutokana na kukwamisha na miundo mbinu ya eneo hilo la
dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.
Meneja wa Dampo la Pugu
Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu ambacho
kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari
(Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo
hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa
huduma ya kuzoa taka mjini.
Devera wa gari la Kampuni ya
usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi akielezea adha
wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika mahali inawabidi kulala siku
mbili na gari zenye mzigo wa taka katika mazingira ambayo ndio
wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza kuwasabishia maradhi hivyo
ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili kuwaepusha na mazingira
hatarishi kiafya kutokana na uchafu unaolundikana mahali pamoja kuanzia
dampo hadi kwenye magari.
Aidha amefafanua kuwa hali hiyo
inasababisha kutuchafulia jina la kampuni yetu na kuonekana kama
hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na
suala la miundo mbinu.
Pia ameshauri jiji liongezewe
uwezo kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu kinachopelekea
kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
Mmoja wa madereva wa magari ya
taka yaliyokwama kutokana na miundo mbinu mibovu Bw. Frank John
akielezea kero ya kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu
Kinyamwezi ambapo amesema taka zimelundikana barabara hazipitiki hata
magreda ya kuzoa hayana pakupita na kuwaomba watu wanaohusika na dampo
kujaribu kutengeneza njia mbadala na kushauri itafutwe njia kipindi cha
Masika taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na kipindi cha Kiangazi kiwe
na sehemu yake na kushauri mamlaka zinazohusika na usafi zijifunze
kutoka kwa wananchi na sisi tujifunze kutoka kwao.
Aidha Bw. John amewataka
viongozi wahusika kutokaa maofisini na kutembelea maeneo husika na
kujiuliza kwanini gari zinakwama na kuongeza kuwa tatizo hilo
limepelekea lawama kwa baadhi kampuni za usafi kushindwa kutekeleza
majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
Hii ndio hali halisi ya viroba
vya uchafu vilivyolundikwa katika eneo la Pugu Kwalala pembezoni mwa
barabara na makazi ya watu ambapo wananchi wamekuwa wakizilalamikia kwa
sababu kipindi cha mvua vinaweza kuwasababishia magonjwa ya milipuko
ikiwemo Kipindupindu.
Mkazi wa eneo la Gongo Mwisho wa
lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau akilalamikia ubovu wa magari ya
taka ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Dar es Salaam na vile vile
utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka ambapo hata kama gari imeharibika
yangetumika magari mengine kuja kubeba taka suala ambalo linalohusu
uongozi wa Manispaa ambao ndio unaogharamia magari yanayobeba taka kitu
ambacho kinaonyesha utaratibu wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia
kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio
dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama
dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya
kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili
ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na
ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli
tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
Mkuu wa Afya Mazingira wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe
akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na tatizo la
mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo la Pugu
Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara unaopelekea
kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa kipindi cha
siku hizi tatu.
Hata hiyvo amesema katika muda
wa siku tatu kuanzia leo Manispaa itahakikisha inarekebisha miundo mbinu
ya kuelekea dampo ili kuweza kupunguza msongamano uliopo wa magari ya
taka yaliyokwama yaweze kurudi mjini kuendelea na ubebaji wa taka.
Aidha Bw. Membe ameahidi kuwa
shughuli za umwagaji taka katika dampo hilo zitakuwa zikifanyika mchana
na usiku ili kuondoa mlundikano wa taka mitaani ambao umejitokeza katika
muda wa siku tatu.












Post a Comment