Multichoice Tanzania yajikita katika kusambaza Digitali katika shule za msingi Tanzania.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni wanahabari katika hafla
mchapalo ya kusheherekea Africa Day na Dstv ambapo amesema DStv inatoa
nafasi kwa wateja wake kuwa na fursa ya kuchagua vifurushi mbalimbali
kulingana na uwezo wa mteja ambacho cha uwezo wa chini kabisa ni Access
chenye zaidi ya channeli 40 gharama yake ni nafuu sana ambapo mteja
atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi. (Picha na Zainul Mzige wa dewjiblog).
Meneja wa Fedha wa kampuni ya
Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akizungumzia malengo ya DStv
Tanzania ambapo amesema wao kama waendeshaji wa biashara nyingine barani
Afrika wanaojali na kuthamini maendeleo ya jamii wameona ni wajibu
kusaidia jamii ili kuweza kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini
Tanzania.
Kwa kuendeleza hilo Multichoice ina
mfumo wa kutoa elimu mashuleni ( Multichoice Resource Centre) hivyo
watamumia jukwaa la Teknolojia kama darasa kwa njia mbalimbali kuwapa
jamii nafasi ya kuendeleza vipaji na ujuzi.
Mfumo huo kutoa rasilimali kwenye
shule kama vile ving'amuzi vya Satellite, VCRs/DVD na kifurushi cha
elimu cha Dstv. Mpaka sasa Multichoice imeanzisha vituo vya rasilimali
jamii katika shule 82 nchi nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya, Pwani na Tanga.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice
Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) akifafanua jambo wakati wa hafla
mchapalo katika kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv. Kulia ni
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu na kushoto ni Meneja
Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi.
Waalikwa katika hafla mchapalo ya
kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv katika Hoteli ya New Africa ya
jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa
Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Blogger John Bukuku wa Fullshangwe
Blog, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Mdau wa DStv
na Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji wakipozi kwa
picha.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) akifurahi jambo Wanahabari Sidi Mgumia
(katikati) na Mama Mhina.
Ronald Shelukindo na Mdau LEMUTUZ wa Blog ya jamii.
Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa
Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo
Ronald Shelukindo, Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis
Senguji na mdau wa DStv wakipozi mbele ya camera yetu wakati wa hafla
ya kusheherekea African Day na DStv iliyowakutanisha waandishi wahabari
kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Bloggers wakishow love...Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John Bukuku, William Malecela
wa Blog ya wananchi a.k.a LEMUTUZ na Operations Manager wa Mo Blog
Zainul Mzige a.k.a Bigzee katika hafla mchapalo ya kusheherekea African
Day na DStv katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa bize kujaza Quiz
iliyotolewa na kampuni ya Multichoice Tanzania ambapo mshindi kwanza
amezawadiwa Full Set ya King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya mwezi
mmoja na washindi kumi wamezawadiwa kofia na T-shirts za Supersport moja
ya chaneli zinazopatikana katika king'amuzi cha Dstv.
Wanahabari wakiendelea kuumiza kichwa huku wengine waki-google majibu ya Quiz hiyo kupitia simu zao za kiganjani.
Mtangazaji wa Radio Dennis Buslwa
a.k.a Ssebo (kulia) akiwa busy kutafuta majibu ambapo tunahisi alikwa
anawasiliana na watu wa Mo Blog wampe majibu kamili. Wengine ni Kamera
Man wa Channel Ten na Mtangazaji wa Radio Salma Msangi pamoja na mdau wa
Star Tv.
Barbara Kambogi akiteta jambo na Angela Msangi wa TBC.
Dada Revina Bandihai wa kampuni ya Multichoice Tanzania na HR Manager wa kampuni hiyo.
Ronald Shelukindo na Dada Furaha Samalu wakifungua mziki wa Kiafrika huku Bw. Francis Senguji akiserebuka na mdau.
Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John
Bukuku akiserebuka na Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara
Kambogi wakati wa hafla hiyo.
Salma Msangi akionekana Kiafrika zaidi akiyarudi na Khadija Kalili wa Jambo leo.
Kwaito ilichezeka kisawa sawa....Chezea Multichoice wewe.....Ilinogaje.!
Kutoka kushoto ni Blogger Cathbert
Angelo wa kajunason Blog, Mpiganaji Fadhili Akida na Blogger Othman
Michuzi wa mtaa kwa mtaa Blog wakipoowz mbele ya kamera yetu.
Bloggers katika picha ya pamoja.
Dada Revina Bandihai wa Multichoice Tanzania na Bw. Francis Senguji wakisataka Rhumba wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Fedha wa Multichoice
Tanzanua Bw. Francis Senguji akimpongeza Ssebo baada ya kuibuka mshindi
katika Quiz iliyoendesha na Kampuni hiyo ambapo alinyakua Full Set ya
King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya mwezi mmoja.
Pichani juu na chini Meneja Uhusiano
wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akigawa Kofia na T-shirts kwa
washindi wa Quiz ilyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa kusheherekea
Africa Day na Dstv.
Dada Revina Bandihai (kushoto) wa Multichoice Tanzania akishow love na washindi wa Quiz iliyoendeshwa na kampuni hiyo.
Wanahabari wakishow love...Thank you DStv for the Cocktail Party to celebrate Africa Day with DStv.





























Post a Comment