Bharti Airtel yasaidia kuondoa umaskini kupitia mradi wa Millenium Village
Meneja
huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea wafanyakazi wa afya wa
mradi wa millenium village wakati akikabithi simcards 240
zitakazowasaidia wafanya kazi hao kuwasiliana kwa bei nafuu na kutoa
huduma kwa wakazi wa Mbola Tabora.akishuhudia ni Mkurugenzi wa mradi huo
Dr Gerso Nyadzi na wafanyakazi wengine wa mradi huo Meneja
Huduma za Jamii wa Aitel Tanzanaia- Hawa Bayumi akikabidhi SIMcard 240
za mtandao huo kwa Meneja Mkuu wa Mradi wa Millenium Village ulioko
Mkoani Tabora- Dr Gerson Nyadzi. Mradi huu unalenga katika kuboresha
huduma za afya na elimu vijijini kupitia technolojia ya mawasiliano.
Kulia ni afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Charles Elisante, na Meneja
wa Airtel money kanda ya ziwa Violet Gyumi. Hafla ya makabidhiano
ilifanyika mkoani Tabora
Mradi huo kutoa elimu kwa wafanyakazi wa afya kwa kupitia
huduma za mawasiliano.
Yawawezesha wafanyakazi 240 kuwasiliana kwa gharama nafuu za pekee.
Airtel unasaidiana na mradi huu wa millennium village katika nchi 6 za
Afrika
Dar
es Salaam Juni 04 2013: Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongoza kwa
kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika ndani ya
nchi 20 barani Afrika na Asia, leo imethihirisha thamira yake ya kufikia malengo ya Millenium kwa
kushirikiana na kampuni ya Erickson katika mradi maalum ujulikanao kama
Millenum village inayoendeshwa katika nchi 6 za Afrika ikiweko
Tanzania.
Mradi huo umeundwa na taasisi ya Earth Institute kwa dhamira ya kutimiza baadhi ya malengo ya Milenia kwa kuelekeza ufumbuzi wa kiubunifu zaidi katika maeneo ya vijijini huku ikishirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni ya simu za mkononi Airtel barani Afrika Airtel imesaidia mradi wa millennium village katika mkoa wa Tabora kwa kutoa huduma za mawasiliano zitakazowawezesha watu kupata elimu kuhusu maswala ya afya kwa urahisi. Airtel imetoa namba ya dharura itakayopigwa bila kutozwa gharama yoyote na kuwawezesha watoa huduma za afya na wagonjwa kuwasiliana kiurahisi zaidi.
Mradi
wa millennium Vilage unasaidiwa na Airtel katika nchi 6 ambazo Airtel
inafanya biashara zake. Nchini Tanzania mradi wa millinium village
umeanzishwa katika eneo la Mbola mkoani Tabora na kusambaa katika maeneo
mengi na kufikia zaidi ya vijiji 20 vilivyopo katika eneo lenye mita
za mraba 700msq likiwa na wakazi 30,0000 waishio katika wilaya ya Uyui
Tabora.
Mpaka
sasa mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa, zaidi ya watu 500,000
katika nchi 11 zilizoko kusini mwa jagwa la sahara Afrika wamefaidika
ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2011 asiliimia 90 ya vijiji vilikuwa vimesha unganishwa
na mtandao wa simu Vile vile ndani ya mradi huu kuna kipengele cha
Connect to Learn, chenye ushirikiano baina ya Earth Institute Chuo
kikuu cha Columbia , Ericsson and Bharti Airtel Africa,
ulioanzishwa katika shule zilizopo ndani ya mradi wa millennium village
na kuwafikia walimu na wanafunzi zaidi ya 5,000 katika nchi za Ghana,
Tanzania, Uganda na Kenya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema” Airtel ina dhamira ya kugusa maisha ya watu si tu kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu lakini pia kuwazifikia jamii za chini zenye uhitaji wa technologia katika kuendeleza na kukuza maisha yao, ambayo ndio lengo lililotufanya kushirikiana na Earth Institute pamoja na Erickson kusaidia mradi huu wa millennium village. Ushirikiano huu unatupelekea kufikia malengo ya mradi wa millennium village ya kushughulikia changamoto za umasikini katika maeneo mengi ikiwemo Kilimo, elimu, afya, miundo mbinu, usawa katika jinsia na kukua kwa Biashara.
Tunafurahi kuwa sehemu ya mabadiliko na tunaahidi kuisaidia jamii nchini Tanzania.
Akiongea
wakati wa halfa ya kupanua mradi wa millennium village katika kijiji
cha Mbola mkoani Tabora, Meneja Huduma Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi
alisema” tunafurahi kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za
mawasiliano zenye gharama nafuu katika vijiji mbalimbali Tanzania . leo tunaonyesha kwa
vitendo dhamira yetu na kuwapatia wafanyakazi 240 huduma za mawasiliano
ili kuuendesha mradi huu wa millennium village kirahisi. Airtel pia
imetoa namba ya dharura ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo huduma za dharura na elimu ya afya katika kijiji cha Mbola”
“Huduma
ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana
simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na
huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii” aliongeza Bayumi Kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika
zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema” ni
imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu
za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa
kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii kupita mitandao na kuongeza
uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule.”
Mbali na mradi wa Millennium Villages , Airtel Tanzania iko mstari wa mbele katika kusaidia shule za secondari nchini kwa kuwapati nyenzo za kufundishia ikiwemo vitabu. Tangu kuanzishwa kwa mradi wa ’Airtel Shule Yetu’ zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na kupata vitabu kutoka Airtel.
Reviewed by crispaseve
on
10:15
Rating:
Post a Comment