Header AD

MSANII SAIDA KALOLE AZUSHIWA KIFO





Jana  kumekuwepo na taarifa kutoka kwa mwanahabari, Frederick Katulanda kupitia kundi pepe la majadiliano la MabadilikoTanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki aliyekuwa maarufu Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia  katika ajali ya kuzama kwa boti.

Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.

Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.

Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”ila  msanii  huyo hakuwepo katika  boti  hiyo na  wala hayupo  wilayani Muleba hivyo  taarifa  hizo  hazina  ukweli wowote na mtandao  huu unamwombea maisha marefu  zaidi msanii Saida Kalole
Reviewed by crispaseve on 10:14 Rating: 5

No comments

Post AD