DADA YAKE “FREEMAN MBOWE” AIKIMBIA CHADEMA NA KUJIUNGA CCM, ADAI CHADEMA HAINA JIPYA.

DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha
Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya
katika chama hicho.
Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda
zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika
Chadema, siyo kwa sababu ya familia.
Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.
Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya
kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana
utashi wake wa kisiasa.
“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu,
ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi
ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala
ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.
Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”
“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani
Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe,
baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa
sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi,
yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa
ushirikiano.
Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai,
Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya
kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.
Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na
kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi
sasa amepokea wanachama 530.
Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo
kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM
katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya
CCM.
Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea.
Post a Comment