Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Dharurua 'Emergency Medicine Profesa, Victor
Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na Meneja wa
Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel
Ondoyo Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza
Na Mwandishi Wetu
MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo
ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya
hospitali ya Taifa Muhimbili .
Msaada huo wa kwanza kutoa inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo
watatoa viti mbalimbali katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa
ajili ya umeme wa jua . Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma
za Dharura 'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru
kampuni ya Chloride Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza
katika kitengo chao kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine
kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo
tunaomba msaada maana hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na
kinategemewa sana kama mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo
Nae Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru
Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo
kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana |
Post a Comment