MAHAFALI YA KWANZA YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA YATIKISA NYAMISATI RUFIJI
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipowasili
katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya
Sekondari WAMA Nakayama yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo katika
kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani jana.Zaidi ya
wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi
mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo ambayo
ilihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri akiwemo balozi wa Japan
na wafanyabiashara ambapo mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi aliahidi
kuisadia shule hiyo shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano
mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano.Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo. Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shule hiyo Dr. Ramadhan Dau. Wahitimu wakiingia katika eneo la tukio Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi. Rais
Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika
meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya
WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania
Mhe.Masaki Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma
Kikwetena kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya
shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.
Shukuru Kawambwa. Baadhi wa walimu wa shule hiyo Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu katibu mkuu taaisis ya WAMA na Dan Kiondo. Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama Mh. Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo
Reviewed by crispaseve
on
08:11
Rating:
Post a Comment