WAHARIRI TANZANIA NI SIKIO LA KUFA ,WACHARAZA WAPEWA DOZI YA BAKORA NA WANAHABARI IRINGA
Mchezaji wa timu ya wanahabari Iringa Lukelo Mkami kushoto akiteta jambo na mlinda mlango wa akiba wa timu ya wahariri
Kikosi cha wanahabari Iringa waliovalia uzi wa yanga
Mgeni rasmi mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Bw Kibanda akizungumza na wachezaji kabla ya mchezo kuanza
Timu ya jukwaa la wahariri kulia
yenye uzi wa simba ikiwa na timu ya wanahabari mkoa wa Iringa kabla
ya mchezo kuanza uwanja wa samora jana
Kikosi cha wanahabari Iringa kilichoanza kazi
Mgeni rasmi katika mchezo huo mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,akisalimiana
na wachezaji wa timu ya wanahabari mkoa wa Iringa katikati ni
katibu wa IPC Francis Godwin akisaidia kutambulisha wachezaji hakuna
mamruki hapa
Kikosi imara kweli kweli japo si wote wapenzi wa Yanga ila voda Com imetuweka pamoja
Kiongozi wa timu ya jukwaa Kulwa
Karedia kulia akimtambulisha mgeni rasmi mwenyekiti wa jukwaa Bw
kibanda wachezaji wa timu yake iliyochezea bakora
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,akiwa na mchezaji wa wanahabari Iringa Lukelo Mkami
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda,
kulia akiwa na wachezaji wa timu zote mbili kabla ya mchezo na
kushoto ni mwalimu wa timu ya jukwaa la wahariri Bw Masoud
Hili ndilo goli la pekee kwa wanahabari Iringa
Wanahabari wakifuatilia mchezo huo
Mlinda mlango wa Jukwaa akiwa hoi baada ya kuchezewa vibaya
Wachezaji wa akiba Swiga Mwaisumbe
kocha wa timu ya wanahabari Iringa na Francis Godwin katikati pamoja
na mbunge Peter Msigwa wakijiandaa kwa kupasha kabla ya kuingia
uwanjani kipindi cha pili
Hapa wachezaji wa akiba Swiga Mwaisumbe kulia ,mbunge Peter Msigwa na Francis Godwin wakipasha
Mzee wa matukio daima jezi nnamba 7
akiwajibika uwanjani baada ya kuingia kipindi cha pili huku mwamuzi
wa mchezo huo Frederick Mwakarebela kushoto akikimbia kuufuata mpira
Washambuliaji hatari mzee wa matukio
daima namba 7 ,mbunge Msigwa namba 2 kushoto na Raymond Francis mwenye
rasta wakiwajibika vema
Mbunge Msigwa akijiandaa kupiga mpira japo hakuweza kuingiza nyavuni
katibu wa IPC Francis Godwin kulia
akiwashukuru wadhamini wakuu Voda Com , Frederick Mwakalebela na Asas
kwa kudhamini mchezo huo katikati ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibandaaliyekuwa mgeni rasmi na makamu Rais wa UTPC Jane Mihanji
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Bw Kibanda baada ya timu ya wanahabari Iringa kushinda mchezo huo .
TIMU ya jukwaa la wahariri wa habari Tanzania (TEF) imekuwa ni sawa na sikio la kufa ambalo kamwe halisikii dawa baada ya kukubali kupokea tiba ya bakora moja kutoka kwa wanahabari mkoa wa Iringa .
katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Samora Iringa jana ,mchezo uliojaa vionjo vya kila aina kutoka kwa timu zote mbili pamoja na mwamuzi wa mchezo huo aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela timu hizo ziliweza kuvunja mbavu za mashabiki uwanjani hapo.
Wakati wachezaji wa timu ya wanahabari Iringa baada yao wakionyesha kujikata chenga wenyewe kwa wenyewe ,timu ya jukwaa ambayo ilikuwa na wachezaji waliokula chumvi nyingi huku baada yao wakishindwa kukimbia kutokana na vitambi walivyokuwa navyo bado kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya timu hizo kuona nyavu ya mwingine.
kipindi cha pili timu zote vilifanya mabadiliko makubwa zaidi kwa kuwatoa wachezaji karibu ya nusu ya wali waliocheza kipindi cha kwanza na kuweka wapya hali iliyoonekana ni ngumu zaidi kwa jukwaa la wahariri na nyepesi kuliko kwa wanahabari Iringa ambao waliweza kutumia mabadiliko hayo kuwacharaza bakora wahariri hao .
Wanahabari Iringa wakicheza kwa nguvu zote kipindi cha pili walipata bao la kuongoza na kufungia dimba dakika ya 3 kipindi cha pili goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Awali katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) mkoa wa Iringa Francis Godwin alisema kuwa mbali ya timu yake kushinda ila ushindi huo ni mwembamba sana na kuwa walipendezewa kuichapa timu hiyo ya jukwaa la wahariri kwa jumla ya magoli 5-0.
Hata hivyo aliwashukuru wadhamini wa mchezo huo ikiwemo kampuni ya simu ya Voda Com kwa kudhamini mchezo huo kwa asilimia 100 ,mdau wa michezo mkoa wa Iringa Frederick Mwakalebela aliyetoa zawadi ya ng'ombe kwa mabingwa wa mchezo huo timu ya wanahabari mkoa wa Iringa pamoja na jukwaa la wahariri kwa kuamua kuja kucheza na wanahabari mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mchezo huo mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alisema kuwa mbali ya timu yake kufungwa ila bado wanahabari Iringa wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa wahariri hao.
Kwani alisema kuwa jukwaa la wahariri kila mwaka limekuwa na mkutano mkuu wa mwaka na kufanyika katika mikoa mbali mbali na mwaka huu wamechagua Iringa kuja kufanya mkutano wao na kucheza mchezo huo wa kirafiki na wanahabari wa mkoa wa Iringa.
Reviewed by crispaseve
on
08:12
Rating:
Post a Comment