MOBILE BANKING YA BENKI YA NBC YAZIDI KUPASUA ANGA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu (kushoto) akimwelekeza
mmoja wa wateja wa benki hiyo, Hangi Donald Kiloba, jinsi ya kupata
huduma za kibenki za NBC kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi (NBC
Mobile Banking) kwenye tawi la benki hiyo la Uhuru jijini Arusha
mwishoni mwa wiki. Wateja wa NBC wanashauriwa kuendelea kwenda katika
matawi ya benki hiyo nchini kote kuunganishwa na huduma hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akimsikiliza
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, John
Mongela wakati mkurugenzi huyo alipofika kwenye ofisi za mkuu wa mkoa
huyo kujitambulisha. Katikati ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa
NBC,William Kallaghe. Bi. Mizinga pamoja na kujitambulisha lakini pia
alielezea mipango na mikakati ya NBC kwa mkuu huyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) akimsalimia mmoja wa
wateja wa benki hiyo, Christopher Cyprian katika tawi la NBC la Uhuru
jijini Arusha. katikati ni Meneja wa tawi hilo, Aliko Mwamusaku .
Mkurugenzi aliwambia wateja tawini hapo kujiunga na huduma za kifedha
za NBC kwa kutumia mitandao ya simu za mkononi (NBC Mobile Banking) ili
kupata huduma za kibenki na pia kufanya malipo ya huduma mbalimbali
kutoka kwa watoa huduma watakaounganishwa na NBC Mobile banking.
Meneja
wa Benki ya NBC Tawi la Uhuru mkoa wa Arusha, Aliko Mwamusaku (kushoto)
akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Mizinga Melu
(katikati) kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Sijohn Chembakassery wakati
wa ziara ya mkurugenzi huyo tawini hapo jijini Arusha.
Mkurugenzi.
mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Mwelu (kushoto),
akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya hiyo, John Mongela wakati mkurugenzi huyo alipometembelea mkuu
huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana, jijini Arusha.
Reviewed by crispaseve
on
10:00
Rating:
Post a Comment