Header AD

Mbio za Rock City Marathon 2013 zafana.

 Mshindi  wa kwanza wa mbio za Rock City Marathon 2013 kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonse Felix kutoka mkoani Arusha akimalizia mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo alitumia saa 1:02:17 na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka jana na Opio Chacha aliyetumia saa 1:05:47.
   Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21kwa upande wa wanaume Alphonse Felix ambaye pia alijinyakulia zawadi ya tiketi ya ndege toka moja wa wadhamini wa mbio hizo Precission Air, ya kuelekea Dar es Salaam na kurudi mkoani kwake Arusha.
  Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental, Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Joel Kimbiaye toka Kenya mara baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili mbio za Rock City Marathon 2013 ambapo pia mshiriki huyo alijinyakulia kitita cha shilingi 900,000/=.
 Afisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta  akikabidhi zawadi ya shilingi 700,000/= mshindi wa tatu katika mbio za Rock City Marathon  kilomita 21, Andrew Sambu ambaye pia alijinyakulia king’amuzi cha Continental.
 Afisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta  akikabidhi zawadi ya shilingi 700,000/= mshindi wa tatu katika mbio za Rock City Marathon  kilomita 21, Andrew Sambu ambaye pia alijinyakulia king’amuzi cha Continental.
   Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 900,000/= mshindi wa pili wa mbio za Rock City Marathon kilomita 21 wanawake Sarah Ramadhan ambaye pia alinyakuwa king’amuzi cha Continental. 
  Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental  Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa mshindi wa tatu mbio za Rock City Marathon 2013 wanawake, Zakia Mrisho ambaye pia alijinyakulia kiasi cha shilingi 700,000/=
    Washiriki wa Rock City Marathon 2013 wakichuana vikali kuisaka nafasi za ushindi wa mbio hizo ili kujinyakulia zawadi mbalimbali zilizoanishwa na wadhamini wa michuano hiyo ambao iliandaliwa na ampuni ya Capital Plus International Limited kwa kushirikaina na wadhamini mbalimbali. 
   Washiriki kutoka Australia wakimaliza mbio za kilomita 21.
Baadhi ya raia wa nchi za kigeni wakipumzika baada ya kumaliza mbio za Rock City Marathon. 
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2, Benedicto Mashauri wa mwanza, baada ya kuwashinda watoto wenzake 284 walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF, akiwa kwenye mstari tayari kuanza mbio za kilomita 5, ya Rock City Marathon iliyoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International, jijini Mwanza jana
Sehemu ya umati uliojitokeza kushiriki mbio za Rock City Marathon 2013.

Reviewed by crispaseve on 09:59 Rating: 5

No comments

Post AD