PROIN PROMOTIONS KUIINGIZA SOKONI FILAMU YA "FIGO"
Kampuni
ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin
Promotions Limited inatarajia kuingiza movie yake nyingine sokoni mapema
wiki hii.
Filamu
ya "FIGO" ni filamu ya kitanzania ambayo imechezwa na waigizaji
wakongwe katika tasnia ya filamu nchini na Ni filamu ambayo inasimimua,
kufundisha na kuelemisha, Filamu ya Figo ni moja kati ya filamu ya
Kitanzania ambayo imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kutengenezwa
kwa hali ya juu na kampuni Mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu
Tanzania ya Proin Promotions Limited.
Proin
Promotions ni moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji,uuzaji na
usambazaji wa filamu Tanzania ambayo tayari ishaingiza Sokoni Filamu
Mbili ambazo zinafanya Vizuri kama vile Foolish Age, Long Time na sasa
inakuletea Filamu ya FIGO ambayo imechezwa na Jennifer Kyaka ambaye
anafahamika kama Odama, Irene Uwoya, Rachel Haule, Stanley Msungu na
wengineo wengi.
Filamu
ya "FIGO" inatarajia kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo
itapatikana katika maduka yote ya Uuzaji wa filamu na Kwa mawakala Wao
Nchini Nzima, Vilevile Unaweza kununua filamu hiyo ya figo kupitia
Ukurasa wa facebook wa Proin Promotions Limited Kupitia https://www.facebook.com/proinpromotions na kupitia pia tovuti yao ya http://www.proinpromotions.com
Pata Nakala yako Sasa
Reviewed by crispaseve
on
09:57
Rating:
Post a Comment