Header AD

OMARI KIMWERI KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA MTANZANIA




omari Kimweri
BONDIA MTANZANIA   OmariKimweri  'Lion Boy' anaefanya shughuli zake Deer Park, Victoria, nchini Australia anatarajia kuwa mtanzania wa kwanza kupanda uringoni  November 30  kugombea ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na  WBC uzito wa kg47.5 minimum weight
Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China   November 30  na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china  xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo

Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa

Omari Kimweri and Randy petalcoria
na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC 

Ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa Kimweri mwenye rekodi  ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3  na mpinzani wake 

  Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja   

Mabondia hawo wote vijana wenye umri mdogo wa miaka 31 wate wawili wakitofautiana mwezi mmoja tu katika kuzalia mpambano huo umekuwa gumzo katika nchi tatu kwa sasa kwani kila mmoja anajiandaa kivyake

Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makari uku akipewa sparng na bondia  Randy petalcoria  wa Philippines ambaye ni bingwa wa  light fly weight 

Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri
Reviewed by crispaseve on 22:55 Rating: 5

No comments

Post AD