Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) nchini Uingereza
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Swissport katika
uwanja wa ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere wakati akielekea kwenye
ndege jioni
ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara
ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa
Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu
wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Meneja wa
Shirika la ndege la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. (PICHA
NA IKULU).
====== ====== =====
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni
ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya
kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali
ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun.
Mkutano huo wa siku
mbili utafanyika keshokutwa Jumatano na Alhamisi kwenye Ukumbi wa Queen
Elizabeth 2 mjini London.
Miongoni mwa mambo makuu
ambayo mkutano huo utazungumzia ni Serikali Uwazi na Ajenda ya Maendeleo Baada
ya Mwaka 2015 wakati muongo wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) unafikia
mwisho.
Masuala mengine
ambayo yatazungumzwa katika mkutano ambao Rais Kikwete anaambatana na Mawaziri
wake watatu ni pamoja na uwazi katika manunuzi ya umma, uwazi katika mikataba,
haki ya kupata habari, uwazi katika ukaguzi wa fedha za umma, uwazi wa Serikali
na vyombo vya habari, uwazi katika mikataba ya maliasili, uwazi katika
maendeleo ya nchi zinazoendelea.
Mawaziri
wanaoambatana na Rais Kikwete katika ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba
Mheshimiwa Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora
Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Mheshimiwa Mwinyihaji Makame.
Rais Kikwete
anatarajia kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 2, 2013.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Reviewed by crispaseve
on
22:54
Rating:
Post a Comment