Header AD

VIGOGO WA CCM WAPATA SHAHADA CHUO KIKUU HURIA

 Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Asha-Rose Migiro, akimpongeza Kada wa CCM, Asha Abdallah Juma, baada ya kumtunuku shahada ya pili ya Biashara ya Chuo hicho, katika mahafali ya 25, yaliyofanyika leo, Makao Makuu ya OUT, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Kushoto ni Makamnu Mkuu  wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette. Asha ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC CCM, amewahi kuwa Wazirikatika serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa NEC ya CCM, Asha Abdallah Juma baada ya wote kutuniwa shahada zao katika mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika jana, Oktoba 27, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani.  Chongolo ametunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya Pili ya Biashara. Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa shahada ya Mawasiliano ya umma.
Reviewed by crispaseve on 23:54 Rating: 5

No comments

Post AD